Na Mwandishi wetu
MAOMBI yanatakiwa kwa mama wa marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa kufuatia hali inayomkuta hivi sasa kutokana na kifo cha mwanaye, Risasi Jumamosi limemfuatilia kwa ukaribu na kubaini matukio kadhaa.
Katika tukio bichi kabisa, mapema wiki hii, mama Kanumba alipata mshtuko uliomsababishia kupandwa na presha baada ya kuingia chumbani kwa marehemu na kukumbana na taswira ya picha ya marehemu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama huyo alishatoa agizo kwa wanafamilia kuzifunika ukutani picha zote za marehemu zilizomo ndani ili asiweze kumwona mwanaye ambaye aliaga dunia ghafla.

Ikasemekana kuwa siku ya tukio la wiki hii, mama Kanumba alifungua mlango wa chumba cha marehemu na kukutana uso kwa uso na picha kubwa iliyokuwa ukutani jambo ambalo lilimshtua sana.
“Alikuwa anaingia chumbani kwa marehemu, ile anafungua tu mlango ukutani akakumbana na picha ya marehemu, akashtuka, presha ikampanda. Maskini, sijui nani aliyeigeuza ile picha wakati mwenyewe alishaamuru picha zote zifunikwe ili asizione,” kilisema chanzo chetu.
Kikaendelea: Tangu alipopata taarifa za kifo cha mwanaye, mama Kanumba amekuwa mtu wa kupandwa na presha, kupoteza fahamu na kutundikiwa dripu, hivyo anatakiwa kuombewa sana.
MLOLONGO WA MATUKIO
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, tukio la kwanza la mama huyo kupoteza fahamu ni lili lillilotokea Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, Aprili 8, mwaka huu alipotua akitokea Bukoba, Kagera ambako ndiko alikopatia taarifa za kifo cha mwanaye. (angalia picha ya ukurasa wa kwanza).

Waombolezaji waliokwenda kumpokea, akiwemo mama wa nyota wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Mary Kigosi walifanya kazi ya ziada kumpatia huduma ya dharura ili arejee katika hali yake ya kawaida.
MAISHA NYUMBANI KWA KANUMBA
Kuna ushahidi wa kutosha kwamba ndani ya nyumba ya marehemu ambapo mama Kanumba yupo kwa sasa, Sinza ya Vatican City Hotel, jijini Dar picha zote za marehemu, hata ile iliyotumika kwenye utambulisho wa jeneza na meza ya viongozi kuandika kitabu cha kumbukumbu, zimefunikwa ukutani.
Ndugu mmoja wa karibu aliliambia Risasi Jumamosi mbele ya mama wa marehemu kuwa mama huyo amekuwa akipata tatizo la presha kupanda mara kwa mara na kutundikiwa dripu ambapo katika moja ya vyumba ndani ya nyumba hiyo kuna chupa za dripu zilizokwishatumika.
ANAISHI KWA USHAURI
Habari zaidi zikasema kuwa, mama huyo ameshauriwa kuishi na maji ya kunywa karibu ili kupambana na tatizo la presha za mara kwa mara.
Watu wa karibu wanasema mara kadhaa mama wa marehemu anakuwa kawaida, lakini linapokuja suala la kumzungumzia mwanaye, hubadilika sura na kuagiza maji au soda ili kujiweka sawa.
“Mara nyingi hataki mambo yanayomhusu marehemu, ikitokea anawahi kusema ongeeni na Seth (akimaanisha mdogo wa marehemu) ili asijiingize kwenye mawazo ya kumuwaza mwanaye.
KINACHOMTESA KWA SASA
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu, mama huyo kwa sasa anateswa na uhaba wa watu, inapotokea hakuna watu wanaoingia zaidi ya yeye na familia yenye watu wasiozidi sita, ndipo anapokubali kuwa mwanaye amefariki dunia na kuzikwa, hivyo hurejesha kilio upya.

STAILI YA KIFO NDIYO INAYOMTESA ZAIDI MAMA
Jumatano ya wiki hii, paparazi wetu alipata nafasi ya kuongea na mwanafamilia mmoja wa marehemu, nje ya nyumba, ambapo alimuuliza maoni ya mama wa marehemu kuhusiana na kifo cha mwanaye ambapo alisema:
“Mama wa marehemu anakiri kifo kipo, lakini kwa mwanaye anaona afadhali angeugua hata kwa siku moja akili ingekubali kuwa kuna kupona na kufa, lakini ile kuzimika kama mshumaa kunamsumbua zaidi.
WITO KWA VIONGOZI WA DINI
Kifo kimeumbwa, lakini kusahau pia kumeletwa kwa wanadamu, hivyo baadhi ya watu wamewataka viongozi wa dini kwenda nyumbani kwa marehemu na kumfanyia maombi mama Kanumba ili Mungu afute kumbukumbu za kifo cha mwanaye haraka.

“SERIKALI ingekuwa inaamini ushirikina, ningemrudisha mwanangu Kanumba, maana najua hajafa, bali amechukuliwa msukule…” hivyo ndivyo alivyoanza kuzungumza Flora Mtegoa au Mama Kanumba ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita aliamua kutoboa siri nzito ya moyoni mwake, Ijumaa Wikienda limeshiba data.
Mama Kanumba aliyaongea hayo nyumbani kwa marehemu, maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa mama huyo kufunguka kwa undani ikiwa ni siku 23 tangu afariki mwanaye Kanumba na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar.
MSUKUMO WA KUTOBOA SIRI
Mama Kanumba akiwa nyumbani hapo na mwandishi wetu, alimpigia simu mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Ayubu akidai ni ndugu wa marehemu kwa upande wa baba mzazi, Mzee Charles Kusekwa.
Kwa wakati huo, Ayubu alikuwa Shinyanga akamuunganisha na mwandishi wetu.
KISA CHAANZA KWENYE MALI ZA MAREHEMU
Akianika kila kitu kwenye simu, Ayubu alianza kwa kudai Baba Kanumba ni kigeugeu kwa familia huku akijua mila za Kisukuma haziendani na matakwa yake.
“Unajua ndugu mwandishi namshangaa anko (Baba Kanumba), anawezaje kugombea mali za marehemu wakati hakumtolea mahari Mama Kanumba? Hii mila amejitungia mwenyewe, Kisukuma hatakiwi kuuliza mali maana hakumtolea mahari mama wa marehemu,” alisema Ayubu.
YALIYOIBUKA KATIKA MAZUNGUMZO
Katika mwendelezo wa mazungumzo hayo, ndipo mazito nyuma ya pazia yakaibuka kwani Mama Kanumba aliweka wazi kuwa kwa sasa mali za marehemu zinamfanya atishiwe maisha na Baba Kanumba.
Aidha, mama huyo wa marehemu alifika mahali akasema kuwa amekuwa akipokea simu za vitisho ambazo zinamtaka akumbuke alipo mwanaye, hivyo akifanya mchezo na yeye atamfuata huko lakini kisa kikubwa kikitajwa kuwa ni mali za marehemu Kanumba.
Mama Kanumba akatoa wito: “Watanzania niombeeni sana, maana natishiwa maisha sasa, naulizwa kama najua alipo mwanangu, nikifanya mchezo na mimi nitakwenda huko.”
Ijumaa Wikienda lilimwelekeza mama huyo kwamba kama anahisi anaishi kwa wasiwasi kufuatia vitisho hivyo ni bora akafungua kesi ili kujiweka salama zaidi. Lakini mpaka tunakwenda mtamboni hatukufanikiwa kupata RB ya kesi hiyo.
KANUMBA ALIONYWA JUU YA KIFO CHAKE
Akizidi kuweka wazi siri nzito, mama huyo wa marehemu alisema mwanaye alijulishwa juu ya kifo chake.
Alisema mtu aliyedaiwa kumpa tahadhari hiyo ni ndugu wa karibu wa Kanumba (jina halikutajwa) akiambiwa kuwa kuna mganga wa kienyeji Shinyanga (jina linahifadhiwa) anatumiwa kuuondoa uhai wake.
Hata hivyo, alisema marehemu alikuwa akidharau kwa vile hakuwa akiamini ushirikina ingawa siku zilivyozidi kukatika, aliamua kuita watumishi wa Mungu na kufanya misa nyumbani kwake, Sinza.
“Kanumba alionywa na ndugu yake mmoja, akamwambia huku Shinyanga si kwema kwako, kuna tetesi kwamba yupo mtu anakuwinda kukutoa roho. Hakikisha unasali sana Mungu akusaidie,” alisema mama Kanumba akimkariri ndugu huyo.
Akaendelea: “Alipuuzia kwa sababu hakuwa mshirikina, lakini kuna siku alifanya misa nyumbani kwake ili Mungu amsaidie kumlinda na shetani huyo na siku chache mbele ndiyo akafariki dunia.”
MGANGA ALIVYOFANYA KAZI
Katika kile kinachodaiwa kuwa Kanumba amechukuliwa msukule, tamko linalotoka kwa mama na kaka wa marehemu ni kwamba mganga mmoja mashuhuri mjini Shinyanga anadaiwa kufika katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kufanya kafara ya kumwondoa Kanumba.
“Unajua tuliambiwa kuwa huyo mtu aliyekuwa akiisaka roho ya marehemu alimwita mganga huyo ambaye alifika nyumbani wiki tatu kabla ya kifo cha Kanumba na kufanya makafara yaliyokuwa na damu na jina la Kanumba.
“Aliyetuambia mchezo mzima alidai kuwa katika kufanya kafara hilo, mganga alichukua damu na kuchora jina la Kanumba huku akisema kuwa haitachukua siku, ataaga dunia,” alisema Mama Kanumba.
MAMA AAMBIWA MWANAYE HAJAFA, WAENDA KWA NABII MWINGIRA
Mama Kanumba aliendelea kuweka wazi kwamba kifo cha mwanaye kilitokea yeye akiwa Bukoba, alipotua Dar kabla ya mazishi, kuna mtu alimpasha habari za kutisha kuwa Kanumba hajafa, kachukuliwa msukule.
Akasema: “Ilibidi Jumatatu (Aprili 9, 2012) tutume wanandugu kwenda Kanisa la Efatha kwa Mchungaji na Nabii Josephat Mwingira kwa ajili ya maombi ya kumrudisha marehemu baada ya kuambiwa alichukuliwa msukule.”
“Mwanangu (mwandishi) ulishawahi kusikia misukule inarudi? Ndicho kilichotokea, hakurudi hata baada ya maombi yale.”
KISA CHA MWILI WAKE KUTOAGWA NA UMATI LEADERS CHABAINIKA
Siri ziliendelea kuvuja, mwanafamilia mmoja naye akasema kuwa pamoja na umati kujitokeza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu, hawakufanikiwa kufanya hivyo kwa sababu za kishirikina.
“Kwa kweli kilichotokea pale kwa watu wanaojua ushirikina unavyofanya kazi wataamini, yule mganga aliyemmaliza Kanumba alifanya kila njia, watu wakawa wanakanyagana, utaratibu ukafa, kwani angeruhusu watu wote kuaga kuna wengine wenye macho ya kiroho, wengine kichawi wangegundua Kanumba wa kwenye jeneza si binadamu,” alisema mwanafamilia huyo (jina linahifadhiwa).
AZIKWA NA BIBLIA
Hili nalo ni jipya, kwani kwa mujibu wa Mama Kanumba, baada ya kuambiwa mwanaye alichukuliwa msukule, familia iliamua kumzika sanjari na Biblia pembeni ili mwili wake usiondolewe kaburini na hao waliomchukua msukule.
BABA KANUMBA NA SIMU YA MWANDISHI
Alipotafutwa Baba Kanumba ili azungumzie tuhuma zilizopo za kutoa vitisho, aliomba kupigiwa baadaye kisha akakata simu.
KIKAO KIZITO SHINYANGA
Habari tulizozipata wakati tunakwenda mtamboni zinadai kuwa Jumamosi, familia ya Mzee Kanumba iliyopo Shinyanga ilikaa kikao kizito cha kumteua msimamizi wa mirathi ya mali za marehemu Kanumba.
Ijumaa Wikienda linaendelea kufuatilia kwa karibu kikao hicho ili kumpata mteuliwa na kumuanika.
No comments:
Post a Comment