Na Joseph Shaluwa
SHINIKIZO la mawaziri waliodaiwa kuvurunda kwenye nafasi zao kuenguliwa linadaiwa kumfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja baraza la mawaziri na kufanya uteuzi mpya.

Wakati hayo yakiendelea, habari zilizotua katika meza ya Risasi Jumamosi zinasema kwamba hali ni mbaya kwa mawaziri waliotajwa moja kwa moja bungeni na wale ambao wanajijua kuwa utendaji wao si wa tija kwa kuanza kujizatiti kabla ya kutimuliwa wizarani.
HAWA ROHO JUU
Mawaziri na manaibu ambao wametajwa bungeni kwa kuhusishwa na utendaji mbovu ni kama ifuatayo:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Huruma Mkuchika, naibu wake Aggrey Mwanri, Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja pamoja na naibu wake Adam Malima.

Mawaziri wengine wanaotolewa macho ni wa Wizara za Uchukuzi inayoongozwa na Omar Nundu na naibu wake Athuman Mfutakamba, Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami na Lazaro Nyalandu (naibu) na Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Hussein Mponda na Dk. Lucy Nkya (naibu).
WASALIMU AMRI
Habari zaidi zinasema mawaziri ambao wanajijua wako hatarini, mbali ya wale waliotajwa bungeni wameanza kufanya maandalizi ya kimya kimya kujiandaa na maisha nje ya wizara kabla ya kupigwa chini.
Chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, kimeeleza kuwa kuna waziri ameondoa picha ya mkewe ofisini kwake akiwa na uhakika kwamba muda si mrefu hatakuwepo.

Mwingine ameanza kuifanyia marekebisho nyumba yake iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar sanjari na kupaka rangi ili akitimuliwa katika ‘mahekalu’ ya mawaziri, aingie huko. Aidha, kuna waziri analifufua gari lake lililoko katika gereji moja ya Wachina, Sinza, Dar.
Waziri mmoja ameikalisha chini ‘nyumba ndogo’ yake kwa kuitahadharisha juu ya matumizi na namna ya kukabiliana na maisha mapya baada ya fagio hilo kupita, wakati mwingine ameahirisha kuchukua mkopo benki kwa kuhofia kushindwa kuurejesha.
TUJIKUMBUSHE
Bunge lililopita, liliwaka moto baada ya hoja kufikishwa mezani juu ya kuwaondoa madarakani mawaziri ambao wameonekana ni wazembe katika utendaji wao. Hata hivyo, bunge liliahirishwa Jumatatu iliyopita bila hatua zozote kuchukuliwa.

No comments:
Post a Comment