Mkoa wa kagera ni mkoa ambao kihistoria una historia nyingi tangu enzi za ukoloni ikiwa ni pamoja na kutoa wasomi hasa profesa wa kwanza alitokea kagera.
Hivi karibuni mara baada ya raisi kutangaza Wakuu wa mikoa wapya mkoa huu ulibahatika kupata Mkuu wa mkoa mpya ambaye kwa idadi tangu kupata uhuru ni mkuu wa mkoa wa 20.
Ukweli ni kwamba sisi Wadau tunampenda sana Mkuu wetu wa mkoa Mh. Kanali mstaafu Fabiani Masawe ila sisi kama wananchi na baadhi ya wadau wa mkoa wetu huu wa Kagera kuna kitu ambacho kinatuchanganya hasa kwenye utekelezaji wa sheria ya kuzima muziki saa 6.
Mkuu huyu bwana wa mkoa alipofika ofisini kwa mara ya kwanza alitangaza kufungwa saa sita usiku show zote za usiku ikiwa ni pamoja na za wasanii na harusi jambo ambalo huko nyumba halikuwepo huku watu wakilia hasara wanayoipata kutokana na kuleta wasanii kutoka nje....au mtu anafuraha yake ya harusi mara ghafla inastishwa na muda.
Maswali yetu sisi wananchi kwa Mh.Mkuu Mkoa :
1. Sheria hii ilikuwa wapi siku zote isitumike?
2. Je!kufungwa kwa show hizi saa sita ni chanzo cha maendeleo ya mkoa?
3. Na je! Kama sheria hii ipo kwa nini mikoa mingine isitekelezwe iweje kagera?
4. Mkuu huyu wa mkoa kabla ya hapo aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya ya kinondoni dar mbona hakutekeleza sheria hii?
5. Ni kweli uhalifu unafanyika usiku tu?
6. Je wadau husika wenye kumbi za starehe wameitwa wakaelezwa azma yako? Hasa ukizingatia kuwa wanalisha watoto na kusomesha kwa kazi hii?
7. Mikoa mingine mbona haitekelezwi hii sheria?
Kinachotushangaza zaidi hata madiwani wetu tuliowachagua kwa maana ya kututetea wamekaa kimya katika hili wakati sisi ni wananchi wao je hawana tamko lolote kuhusu hili, Ikumbukwe sakata la kufunga vijiwe vyote vya kahawa na sheria hiyo hatujui ilihishia wapi kwanini swala hili la kumbi za Starehe na harusi lisifanyiwe ufumbuzi.
Kibaya zaidi hata meya wetu kipenzi tunayempenda ANATORY AMANI amekaa kimya katika hili hapa ukweli mnatupa mashaka viongozi wetu.
Hatupingani na agizo la Mkuu wa mkoa ni kweli sheria ipo, lakini sheria hii ilikuwa wapi siku zote? Na je kabla ya utekelezaji wananchi wameambiwa
Ahsante.
Sisi wadau wa mkoa wa Kagera
No comments:
Post a Comment