Waziri wa Kazi na Ajia, Mh Gaundentia Kabaka, akimkabidhi ngao, Mkurugenzi Mtendaji wa Songas,baada ya kampuni ya Songas kuwa Mshindi wa kwanza katika sekta ya nishati na pia mshindi wa jumla wa mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Ukumbi wa Mliman City Dar es salaam
wafanyakazi kutoka kampuni ya Geita Gold Mine wakifuatilia kwa umakini, baadhi ya maada ambazo zilikuwa zikijadiliwa na wataalamu wa usalama na afya sehemu za kazi, kutoka ILO,OSHA, na watalaamu toka chuo kikuu cha Dar es salaam,
mmoja wa washiriki wa maonesho ambayo yalikuwa yakieendelea sambamba na maadhimisho ya siku ya usalama na Afya duniani, akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa maonesho toka kwa Waziri wa kazi na Ajira, Mh Gaundentia KabakaWaziri wa Kazi na Ajira katikati akiwa na washindi mbalimbali wa TUZO maalumu, iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya usalama na Afya duniani Kitaifa Mlimani City Dar es Salaam,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa ILO hapa nchini ndugu Alex Musindo, wa pili kushoto mstari wa nyuma ni Dr Makongoro Mahanga na Katibu mkuu wa Wizara ya kazi na ajira ndugu Eric Shitindi, pamoja na wajumbe wa bdoi ya ushauri wa wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHAA) na Mtendaji mkuu wa OSHA Dr Akwilina Kayumba.
duniani kote, wafanyakazi huadhimisha siku ya usalama na afya duniani, siku hii ni maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka ndugu zetu waliopatwa na magonjwa ajali ama kupoteza maisha wakiwa makazini.OSHA ambayo wakala mwenye wajibu wa kusimamia sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi iliandaa kongamano la wataaluma mbalimbali kuhusiana na siku hii maalumu
No comments:
Post a Comment