Tuesday, April 17, 2012

WIGAN YAINYUKA ARSENAL KWAO EMIRATES!

WENGER-SITABWAGA_MANYANGA 
Klabu iliyokuwa ikisuasua na sasa imeanza kuzinduka ili kujinasua balaa la kuporomoka Daraja, Wigan, baada ya kuitungua Manchester United bao 1-0 Jumatano iliyopita huko DW Stadium, jana ikiwa ugenini Uwanjani Emirates iliichapa Arsenal bao 2-1 kwenye Mechi pekee ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana.


Breaking the deadlock: Wigan's Franco Di Santo pounced in the 7th minute
 Wigan's Franco Di SantoAkiifungia timu yake goli dakika ya 7

Ushindi huo umewafanya Wigan kupanda nafasi moja na kukamata nafasi ya 16 wakiwa na Pointi 34.
What a week: After beating Manchester United on Wednesday, Roberto Martinez's side won at the Emirates
wiki ya ajabu kwa Wigan, Roberto Martinez'sakifurahia ushindi jana kwa kuwapiga Arsenal

Wigan walipata bao zote mbili ndani ya Dakika moja kwa Franco Di Santo kufunga Dakika ya 7 na Jordi Gomez kupiga bao la pili Dakika ya 8.
No mistake: Thomas Vermaelen gets Arsenal back in the game after nodding in Tomas Rosicky's cross
 Thomas Vermaelen alipiga kichwa na mpira ukaelekea nyavuni ikawa 1-2
Thomas Vermaelen aliipatia Arsenal bao lao katika Dakika ya 21 lakini licha ya kutawala walishindwa kugeuza matokeo ya Mechi hii.


MSIMAMO (Timu za chini:)
 
15 Aston Villa Pointi 35
16 Wigan Mechi 34 Pointi 34
17 QPR Mechi 34 Pointi 31 [Tofauti ya Magoli -19]
---------------------------------
18 Bolton Mechi 32 Pointi 29
19 Blackburn Mechi 34 Pointi 28
20 Wolves Mechi 34 Pointi 23


VIKOSI
Arsenal: Szczesny; Sagna, Djourou, Vermaelen, Andre Santos; Song, Arteta; Walcott, Rosicky, Benayoun; Van Persie
Akiba: Fabianski, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Squillaci, Gervinho, Gibbs, Chamakh.
Wigan: Al Habsi; Alcaraz, Caldwell, Figueroa; Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour; Moses, Di Santo, Gomez
Akiba: Pollitt, Ben Watson, McManaman, Sammon, Jones, Diame, Stam.
Refa: Andre Marriner


RATIBA:
Jumamosi Aprili 21
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Chelsea
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Sunderland
Blackburn v Norwich
Bolton v Swansea
Fulham v Wigan
Newcastle v Stoke
[Saa 1 na Nusu Usiku]
QPR v Tottenham
Jumapili Aprili 22
[Saa 8 na Nusu Mchana]
Man United v Everton
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v West Brom
Wolves v Man City

No comments: