Sunday, May 6, 2012

CHELSEA YATWAA UBINGWA KOMBE LA FA UINGEREZA


KLABU ya Chelsea imetwaa Kombe la FA hivi punde tu, kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuifunga mabao 2-1 Liverpool.
Shukrani kwao, Ramires na Didier Drogba walioifungia mabao hayo Uwanja wa Wembley  jioni hii, wakijiandaa kuwa mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Ujerumani.
Ramires alifunga bao la kwanza baada ya makosa ya Jay Spearing kabla ya Drogba kufunga la pili na Andy Carroll aliyetokea benchi kuifungia Liverpool la kufutia machozi kwa kutumia makosa ya John Terry.
Lakini Liverpool ni kama walinyimwa bao la kusawazisha na refa baada ya mpira uliopigwa na Carroll kuonekana kabisa umevuka mstari wa goli, lakini refa akachomoa.

No comments: