Saturday, June 23, 2012

SIRI IMEFICHUKA: MCHEZAJI WA GHANA AKIRI UDANGANYIFU WA UMRI KWENYE TIMU ZA TAIFA

Tabia ya wachezaji wa kiafrika kudanganya umri imezidi kukitihiri kwenye soka.

Mchezaji wa zamani wa kikosi cha under 17 cha Ghana Yaw Preko amekiri kwamba ni kweli amewahi kudanganya umri wake, na kwamba wachezaji wengi waliowahi kucheza michuano ya FIFA ya vijana wamekuwa wakidanganya umri wao halisi.

Preko pamoja na kukiri kudanganya umri, ameiambia Liquid Sports kwamba suala la kudanganya umri sio jambo geni kwenye timu za taifa hasa barani Afrika na Amerika ya kusini.

"Waafrika tunaongoza na hata kwenye bara la South America hakuna nchi ambayo haifanyi udanganyifu wa umri. Nakumbuka tulipocheza nchini Qatar mwaka 1991, tuliona kama tunacheza na timu ya ligi kuu ya England."

Na vipi kuhusu yeye mwenyewe? Alijibu: "Ndio, siwezi kudanganya, sikucheza soka kwa kusema umri wangu sahihi, japokuwa sikupunguza miaka 20 kwenye wangu wa ukweli."

"Kwenye zama zetu chama cha soka ndio kilikuwa kinatupangia umri, tulifanikiwa sana kudanganya juu ya umri wetu ndio maana nilifanikiwa kucheza 17 barani ulaya."

Preko alikuwa mmoja ya wachezaji waliounda kikosi cha Black Starlets kilichoshinda kombe la dunia chini ya miaka 17 mwaka 1991, na pia kile cha Black Meteors kilichocheza kwenye Olympic Games mwaka 1992.

No comments: