Saturday, July 7, 2012

MAKUBWA YANAYOENDELEA MAHOSIPITALINI

Tangu uhuru bajeti zetu ni kuimarisha afya ya akina mama na watoto je picha hii inatuonyesha nini hasa katika kipindi hiki cha mgomo wa madaktari?? Naona muda wa siasa uishe sote bila kujali itikadi tuanze kuijenga inchi yetu tunakoelekea ni kubaya sana wapendwa siasa imeshindwa kutukombo.
Ni hali halisi inayoendelea katika hospitali zetu za mikoa na hata wilaya.Hakina mama na watoto wanaangaika sana hasa pale wanapokuwa ni wajawazito au watoto wanaumwa.Tuna kila sabaubu kuiomba serikali yetu iwaangalie kwa jicho la huruma akina mama wajawazito na watoto kwani hali ni mbaya mno.
Swali la uzushi.
Je bajet ya nchi inalenga sana barabara kuliko afya za mama zetu?
Je bajeti ya nchi inalenga sana posho ya wa Wabunge kuliko walezi wa Taifa?
Ni kwanini selikari itumie magari ya gharama kubwa badala ya kujenga na kuboresha guduma za afya??????
Ina maana gani kunawa usoni wakati ndani ni uchafu mtupu(kuvaa ngozi ya kondoo wakati una moyo wa chui)

No comments: