Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager,Bwa.Allan Chonjo akimkabidhi Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro,ufunguo wa gari aina ya FORD FIGO mara baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO,inayoendeshwa na kampuni ya bia ya SBL.Pichani kati ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya SBL wakishuhudia tukio hilo lililofanyika mapema leo asubuhi kwenye ofisi ya Kampuni ya CMC,jijini Dar es Salaam
Gari aina ya FORD FIGO aliyojishindia Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro
Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro akizungumza mbele ya Wanahabari mara baada ya kukabidhiwa gari yake,kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager,Bwa.Allan Chonjo
*******
KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAKABIZI GARI MPYA AINA YA FORD FIGO KWA MSHINDI WAKE.NI KATIKA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL.
July 3, 2012, Dar Es Salaam: Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni ijulikanayo kama vumbua hazina chini ya kizibo. Promosheni hiyo inaendeshwa nchi nzima ambapo katika droo ya nne iliyochezeshwa katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar Es Salaam alipatikana mshindi wa gari mpya aina FORD FIGO aliyefahamika kwa jina la Isack Juvenary mwenye umri wa miaka 25 mkazi Morogoro.
Leo asubuhi katika ofisi za CMC zilizopo barabara ya azikiwe mkabala na jengo la maktaba square jijini Dar Es Salaam, mamia ya watanzania kupitia vyombo vya habari wameshuhudia kampuni hiyo ikimkabidhi zawadi hiyo ya gari mshindi wake bwana Isack Juvenary jiji Dar es Salaam.
Akiongea na wandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager Bw. Allan Chonjo amesema “Najisikia faraja kubwa sana ninapoona yale tuliyoyapanga kuyatimiza kwa wateja wetu kama SBL na kwamba hii ni sehemu tu ya yale yoye tuliyopanga kufanya kwa jamii inayotuzunguka kwa kuthamini mchango wa wateje wetu na pia sisi tumelenga katika kuwapa mabadiliko katika maisha yao kwa kuzingatia mahitaji muhimu ya binadamu,
No comments:
Post a Comment