Sunday, August 19, 2012

SIKUKUU YA ID EL FITRI YAANZA KWA AJALI IRINGA


Wananchi wa manispaa ya Iringa wakishuhudia ajali hiyo ya michezo ya pikipiki
Pikipiki na majeruhi wa ajali hiyo wakiwa katika gari ya polisi tayari kwa kwenda polisi
Huku kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akiwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabara kwa siku hii ya leo wakati wa sikukuu ya Id El Fitri ,hali imekuwa tofauti katika manispaa ya Iringa baada ya kijana mmoja aliyekuwa katika maonyesho ya pikipiki kupata ajali eneo la stendi kuu ya mkoa wa Iringa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 8 mchana baada ya kijana huyo mwendesha pikipiki kushindwa kuimudu pikipiki yake hiyo na kumponyoka na kwenda kuwagonga watu wawili waliokuwa wakipata kinywaji katika duka moja eneo hilo la stendi kuu.

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa kijana huyo ambaye alikuwa katika msafara wa waendesha piki piki zaidi ya watatu ambao walikuwa wakizunguka mitaani na kuonyesha vionjo kwa wananchi kabla ya kwenda uwanja wa Samora ambako walipanga kufanya onyesho hilo alijikuta akitupwa chini na piki piki hiyo baada ya kutaka kusimama juu ya stelingi ya pikipiki hiyo huku ikiwa katika mwendo mkali.

Hata hivyo katika ajali hiyo kijana huyo ambaye jina lake bado kufahamika amejeruhiwa pamoja na watu wengine wawili waliokuwa wakishuhudia mchezo huo .

No comments: