Friday, August 24, 2012

Wanachama wa Klabu ya Gymkhana Wamtimua Ali Mafuruki.

 Ali Mafuruki
--
Wanachama wa klabu ya Gymkhana Jana walimuondoa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ali Mafuruki na viongozi wenzake na kuundwa kamati ya muda inayokaa madarakani hadi Septemba mwaka huu.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya viwanja Gymkhana Dar es Salaam, walifikia uamuzi wa kumuondoa Mafuruki kwa kuiendesha klabu hiyo kibabe na kuondoa taratibu nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wanachama.

Hali iliyomfanya mmoja wa wanachama wa klabu hiyo, ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), hasiwe mbiashi kujiondoa kwani hasifanye Gymkhana kama Woorlworth ambayo ni moja ya kampuni anazomiliki Mafuruki.

Kufuatia uamuzi huo, wanachama hao wameteua kamati ya muda itayayoongozwa na Victor Kimesera na Makamu wake Erard Mutalemwa,  huku manahodha wa michezo yote wanendelea na nyadhifa zao ambao ndio wanaounda kamati ya utendaji ya Ghymkhana.

Mkutano huo ulianza saa moja na nusu jana usiku huku kukiwa na polisi waliokuwa na lengo la kulinda usalama, lakini ulitawaliwa na jazba ya kumtaka Mafuruki ajiuzuru kwa madai kuiendesha klabu hiyo kinyume na taratibu na maamuzi mengi yamekuwa yake binafsi.

Hata hivyo, Mafuruki baada ya kuingia katika mkutano huo aliwaambia wanachama hao kuwa mkutano huo haukufuata taratibu hivyo maamuzi yoyote ambayo watayachukua yatakuwa yamekiuka katiba ya klabu hiyo na kususia kikao na kuondoka.

Wakati akiondoka wanachama hao walikuwa wakizome, hali iliyofanya mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo Jaji mstaafu, Stella Longway kuchukua jukumu la kuendesha kikao kwa mujibu wa katiba yakbu hiyo na wanachama kufukia maamuzi ya kuwaondoa viongozi wote wa klabu hiyo.

Klabu hiyo mbali na Jaji Stella inawadhani wengine wawili ambao ni G. Kilindu na Ritha Akena.Wadhamini hao wana mamlaka ya kufanya kazi hiyo kwa niaba ya wanachama wa klabu hiyo.

Kufuatia uamuzi huo, kamati hiyo ya muda inayoongozwa na Kimesera inatarajia kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ni kurudisha ada ya mgeni mwalikwa ‘Guest Fees” kutoka shilingi 10,000/= hadi 2,000/= kama zamani.

Hatua nyingine ni kurudisha utaratibu wa timu za Gymkhana kualika timu za nje kucheza mechi, hali ambayo uongozi wa Mafuruki ulipiga mafuruku kucheza mechi ndani ya viwanja hivyo au timu zinazokuja kulipiwa shilingi elfu 10 kwa kila mchezaji.

Mbali na Mafuruki kama Mwenyekiti, wengine ni

 Makamu Mwenyekiti - Profesa Primo Carneiro; 
Katibu - Nicholas Siwingwa; 

Mweka Hazina - Nada Margwe; 

Mkuu wa Wanachama - Santosh Gajjar;

 Mkuu wa Viwanja - David Shambwe; 
Mkuu wa Bar -  Alfred Kinshwaga

 Mkuu wa Kitengo cha Burudani -  Joseph Kusaga.

Wengine ni manahodha michezo yao kwenye mabano ni 


Joseph Tango (Golf), 

Inger Njiru (Tennis), 

 Chukkapalli Sriram (Cricket),  Ivan Tarimo (Soccer), 
Deepak Dosh (Squash) 

  Firoz Yusufunali (Snooker).

Lakini wanachama hao wanakusudia kuwarudia wakuu wa vitengo vyote kasoro nafasi ya Mwenyekiti. 
 Taarifa na 
E. Mutalemwa
Hii

No comments: