HIZI NDIO MBINU ZILIMFANYA RAMIRES AIMUDU LIGI NGUMU YA ENGLAND
Pamoja na kuwa na umbo dogo mchezaji wa
Chelsea Ramires amekuwa ni mmoja ya wachezaji wachache wageni
waliofanikiwa kuupatia mchezo wa ligi kuu ya kiingereza ndani ya kipindi
cha muda mfupi aliokaa na timu hiyo. Anaonekana ni mchezaji mapafu ya
mbwa, mwenye kujituma vilivyo kwa ajili ya kuipigania timu yake, pamoja
na kuwa na mwili mdogo Ramires amekuwa na uwezo wa kupambana na mijitu
iliyoshiba inayocheza kwa nguvu kwenye ligi kuu ya England. Amewezaje
kuweza kuimudu vizuri EPL? Ramires anaelezea mbinu zake.
1: CHEZA KIBABE
Nilipofika England kwa mara ya kwanza.
Nilikuwa nikicheza nadondoka kila mara na nikagundua kwamba mashabiki
walikuwa wanachukizwa na jambo lile. Lakini sikuwa najiangusha , bali
nilikuwa sijazoea ile hali ya mchezo wa kiingereza. Kama unavyoniona
sina nguvu sana, hivyo nikagundua ili kuwatisha wapinzani wangu inabidi
nicheze kibabe. Baadae nikagundua haisadii sana kwa sababu inakuwa kama
unaanzisha ugomvi. Kama ukicheza kibabe na yeye atakurudishia na hali
itaendelea mpaka mwisho, lakini inasaidia kuwaonyesha kwamba japokuwa
una mwili mdogo hawawezi wakakuonea kwenye kupambana dimbani.
2: JARIBU KUTOKUWA NAO KARIBU WAPINZANI
Kama ambavyo naitumbua sina nguvu sana,
ikiwa nitapokea mpira huku mpinzani wangu akiwa nyuma yangu nitajitahidi
kadri niwezavyo kutoa pasi mapema iwezekanavyo. Najaribu kuzuia
kucheza huku mgongo wangu ukiangalia nyuma kwenye goli - kwasababu ni
bora zaidi kucheza huku ukiwa unatazamana na mpinzani wako.
Ikiwa nahitajika kufanya marking kwa
mchezaji ambaye ana nguvu kuniliko, nafahamu kwamba ni vizuri
kutokalibiana nae na kujaribu kutumia mikono yangu, vinginevyo
atanikumba. Hivyo najaribu kuwapa nafasi na kusubiri muda muafaka
kumuingia kwa kushtukiza. Siwezi kushindana nao kwa nguvu, hivyo
natumia wepesi wangu kama njia mbadala ya kuwashinda.
3: KULA CHAKULA VIZURI NA KUPUMZIKA VYA KUTOSHA
Lishe bora na mapumziko ni muhimu sana
katika kuwa na nguvu. Kabla ya mechi mara zote huwa nakula tambi, samaki
au kuku, na siku moja kabla ya mechi na siku ya mechi huwa nakunywa
maji mengi kuliko kawaida. Hii imekuwa tabia yangu kwa muda mrfu sana na
kuna baadhi ya wachezaji wenzangu wananitania sana kuhusu hili, lakini
siku zote imekuwa inanisaidia na najihisi kujiamini sana, hivyo kwanini
nibadilishe mfumo huu au nibadilishe diet yangu? Baada ya mazoezi,
naenda moja kwa moja nyumbani kupumzika vya kutosha, muda mwingine
nikijifurahisha na video games au kuangalia filamu. Hili jambo ni muhimu
sana kwangu, na lazima kila siku ya mungu nilale kwa muda wa masaa
yasiyopungua nane."
No comments:
Post a Comment