Mmoja
wa wageni rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri
wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akitoa hotuba wakati wa
uzinduzi wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus.
Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye wameingia katika kijiji cha Maisha Plus.
NMB
inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na
kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya
njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.
Vilevile,
NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa
matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu
huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya
kifedha na mengine mengi.
Washiriki wa shindano la Maisha plus wakifuatilia uzunduzi huo huku wakiburudika kwa kinywaji cha dafu.
Naibu
Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman
wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili
jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati)
pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Monica Gorman (kushoto)
akiteta jambo na Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy
Mwalim (kushoto) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw.
Imani Kajula.
No comments:
Post a Comment