Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wafanyakazi wa kiwanda hicho ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa kwa usalama wao ,walidai kuwa wakati wa ziara ya madiwani hao uongozi wa kiwanda hicho ulilazimika kufunga kiwanda kwa muda ili kupisha ziara hiyo kutokana na mazingira ya kiwanda hicho kuwa machafu.
Kwani walisema kuwa kwa kawaida mazingira ya kiwanda hicho ni machafu zaidi na kuna haja ya viongozi hao wakiwemo madiwani wa Manispaa ya Iringa kujenga utamaduni wa kufanya ziara za ghafla katika viwanda hivyo ili kuona hali halisi badala ya kufanya ziara zenye taarifa kama hiyo iliyofanyika na kupelekea uongozi wa kiwanda hicho kujiandaa kwa usafi zaidi.
Wafanyakazi hao walisema harufu mbaya ya uchafu iliyomo ndani ya kiwanda hicho hata wao wafanyakazi imekuwa ikiwaweka katika wakati mgumu ila madiwani walikubali kudanganywa kwa zawadi ndogo ndogo walizopewa wakati wa ziara hiyo na kuwa kuna haja ya madiwani hao hasa kamati ya afya na mazingira kufika kufanya ukaguzi katika kiwanda hicho na viwanda vingine mjini Iringa .
No comments:
Post a Comment