Saturday, November 17, 2012

Pambano La Masumbwi...!

Lile pambano la ngumi kati ya mwaite juma na Baina mazola limekamilika na kesho watazipiga katika ukumbi wa DID mabibo ambapo pia shughuli za upimaji zilifanyikia hapo chini ya oganaizeshen ya ngumi za kulipwa nchi[TPBO] zikisimamiwa na ibrahim kamwe"bigright" akisaidiwa na said chaku,kuhakikisha zoezi zima la upimaji linakwenda sawa.
 
akilizungumzia pambano hilo ndugu mzazi anaeleza kuwa maandalizi yote yapo kamili na mabondia wote wapo vizuri na wana hari ya uzipiga iliyobaki ni kusubiria hiyo siku tu.
 
naye kwa upande wake katibu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE"Bigright" amethibitisha kukamilika kwa asilimia kubwa ya maandalizi ya pambano hilo mabondia wapo katika afya njema na kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kati ya ISSA OMARI atazipiga na JAMES MARTINE, FARAJA SAID"TORES" atapigana na JUMA ALI,nae HERMAN RICHAARD SHEKIVULI atapimana ubavu na OMAR RAMADHAN,huku MPOLE MCKENZIE na ADAM BARNABAS nao watakuwepo ulingo kwa kudundana.
 
Zaidi ya mapambano hayo pia kutakuwepo na maonesho mengiyo ya sanaa za ngumi za watoto

No comments: