Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta
ya Elimu nchini uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China leo.
Katika Mradi huo wa
Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari
na Vyuoni kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma
mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya HUAWEI kutoka China Bw. Bruce Zhang akizungumza katika hafla
hiyo kwamba Mpango huu unaoitwa "Huawei ICT Star" itasaidia katika
shule za Primary na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi
na Teknolojia nchini Tanzania.
Alisema katika Program
hii itasaidia kuboresha miundo mbinu katika Sanyansi na Teknolojia ili
kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na
Teknolojia.
Balozi wa China nchini
Tanzania Mh. LU YOUQING akitoa maelezo yake wakati wa uzinduzi wa
mpango wa Teknohama katika shule na vyuo nchini Tanzania.
Balozi alisema mpango
huu ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu
wa China katika nyanja mbalimbali za biashara uchumi na Kijamii.
Aliongeza kwamba
Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya
Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.
Meza Kuu.
Mgeni rasmi Mh. Mbarawa na Balozi wa China wakizindua rasmi mpango wa "HUAWEI ICT STAR" nchini Tanzania.
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI
Bw. Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya
Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
Profesa Mbarawa akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI.
Pichani Juu na Chini ni wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Waziri Mbarawa akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi.
No comments:
Post a Comment