Saturday, November 3, 2012

Polisi wa Nigeria wauwa wahalifu 14

Polisi wa Nigeria


Polisi wa Nigeria wanasema wamewauwa wafuasi 14 wa gengi la wahalifu ambalo limehusika na utekaji nyara na wizi.
Msemaji wa polisi alieleza kuwa kiongozi wa gengi hilo, ajulikanaye kama Bishop Nelly, ni kati ya wale waliouwawa wakati polisi walipovamia maficho ya gengi hilo katika jimbo la Rivers State, eneo lenye utajiri wa mafuta nchini Nigeria.
Hapo awali gengi hilo lililipwa kikombozi na lilimwachilia huru raia mmoja wa Uturuki aliyetakwa nyara mwezi uliopita.
Polisi wanasema piya wameteka silaha nyingi, risasi na pesa.

No comments: