Friday, November 2, 2012

WENGER AWAOMBA MASHABIKI WA ARSENAL KUMUHESHIMU VAN PERSIE.


KOCHA wa klabu ya Arsenal amewaomba mashabiki wa timu hiyo kumuheshimu mshambuliaji nyota wa Manchester United Robin van Persie wakati timu hizo zitapokutana kesho katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza ukiwa ni mchezowa kwanza nyota huyo kukutana na klabu yake ya zamani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Uholanzi amewahi kucheza katika klabu ya Arsenal kwa kipindi cha miaka nane kabla ya kuhamia Manchester United msimu uliopita kwa ada ya paundi milioni 24. Arsenal itasafiri kuelekea Old Traford ambapo Van Persie anategemewa kurejea katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo baada ya kupumzishwa katika mchezo wa Kombe la Ligi ambao walipoteza kwa Chelsea Jumatano. Wenger amesema kuwa hajui mashabiki wa Arsenal watampokea vipi Van Persie lakini anategemea watamuheshimu kwasababu amewatumikia kwa kipindi cha miaka nane na alikuwa akifanya vizuri. Mara ya mwisho vijana wa Wenger kutua Old Traford walipokea kipigo kitakatifu cha mabao 8-2 kitu ambacho Wenger hatarajii kama kitajirudia tena katika mchezo wa kesho

No comments: