Thursday, December 13, 2012

MAISHA BORA YANAWEZEKANA KAMA VIONGOZI WENGEKUWA NA MOYO WA KUTAMBUA MAISHA BORA KWA WENGINE

MBUNGE KABATI AKABIDHI MIKOPO YA MAMILIONI MANISPAA YA IRINGA


Mbunge wa viti maalum Litah Kabati akimkabidhi hundi mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha wachapakazi Jerida Mlimbila hundi yenye thamani ya tsh. 1m

Mbunge wa viti maalum Litah Kabati akimkabidhi hundi mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha Matunda Prisca Temba hundi yenye thamani ya tsh. 1m

Baadhi ya wawakilishi wa vikundi viliko katika manispaa ya iringa vilivyopata mkopo

  mbunge wa viti maalum Litah Kabati akizungumza na wanakivikundi baada ya kuwakabidhi hundi katika ukumbi wa manispaa)

Mbunge  wa  viti maalum (CCM) mkoa wa Iringa Ritta Kabati amekabidhi mikopo ya mamilioni ya shilingi kwa  vikundi vya manispaa ya Iringa.

Mikopo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia mpango wake wa kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia na kukuza mitaji kwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na kinamama kupitia vikundi mbali mbali leo wametoa mikopo kwa vikundi 11 vilivyoko katika manispaa hiyo yenye thamani ya sh.10.8 fedha ambazo zinatolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Manispaa Theresia Mhongo leo katika ukumbi wa Manispaa amesema kwamba kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 wamepokea kiasi cha shilingi 20m kwa ajili ya kukopesha vikundi vya kiuchumi na kutoka mwaka 2009 mpaka desemba 2011 mfuko umeweza kutoa jumla ya tsh 37m ikiwa ni fedha za mkopo na riba,"jumla ya vikundi 46 vyenye wanachama 414 vimenufaika na kwa kukuza mtaji na kuendeleza biashara ndogondogo wanazofanya na katika ya vikundi hivyo 38 vimemaliza mkopo na kufanya marejesho kuwa sawa na asilimia 82 na vile ambavyo bado vinaendelea kufatiliwa" alisema Mhongo

Kwa  mwaka wa fedha wa 2012/2013 kulikuwa na maombi 28 ya vikundi mbalimbali wenye thamani ya tsh 54.1m ambavyo vinafanya shughuli za ufugaji wa kuku, ng'ombe, nguruwe, biashara ndogondogo na kukopeshana hivyo kamati ya wilaya ilipitia maombi yote 28 na kuona shughuli za vikundi hivyo wanazofanya na kufanikiwa kupata vikundi 11 kwa awamu ya kwanza yenye thamani ya tsh 10.8m na awamu ya pili kutakuwa na mikopo yenye thamani ya tsh. 14m itatolewa kwa vikundi 14.
Akikabidhi hundi katika vikundi hivyo mgeni rasmi na Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi Mh Lita Kabati amesema kwamba wanavikundi wanatakiwa kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyoombea na kuweza kukuza kipato chao, aidha waweze kutunza vizuri fedha. 
"nitawaletea walimu wa ujasiliamali kuweza kuwafundisha na kujifunza jinsi ya kutunza fedha kuongeza kipato na kuwa na malengo ya kuwa na mitaji mikubwa zaidi na ukimwezesha mwanamke ni sawa na kuongeza maendeleo kwa jamii" alisema Kabati

Vikundi kumi na moja vilivyofaidika na awamu ya kwanza ya mkopo huo ni kikundi cha wanawake Ebeneza waaliopata mkopo wa sh. laki 8, kikundi cha wanawake cha Mivinjeni(1m) kikundi cha wanawake cha wachapakazi(1m) Tumaini Group(1m) aidha vikundi vingine ni kikundi cha wanawake cha Matunda cha kata ya makorongoni wao walipata mkopo wa tsh 1m, kikndi cha wanawake cha Lugano (1m) Furaha (1m) Mshikamano wao walipata tsh 1m, kikundi cha wanawake cha Tuhegelye (tsh 1m) Kikundi cha Umoja(1m) na kikundi cha Agape walipata mkopo wa milioni moja na jumla ya mkopo kwa vikundi vyote ni milioni 10. 8 

Katika utoaji wa mikopo hiyo vikundi vyote upatiwa kwanza mafunzo ya bishara ili kuweza kutunza kumbukumbu na uambatana na ujazaji wa mkataba wa makubaliano ya kiasi kilichokopeshwa na marejesho kwa mwezi na mwisho wa marejesho.

No comments: