TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU
WA RAIS WA JAMHURI YA MUUUNGANO WA TANZANIA DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL
AMUWAKILISHA RAIS KATIKA SHEREHE ZA KUMUAPISHA RAIS ENRIQUE PENA NIETO WA
MEXICO
Mexico
City,
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
amemuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Enrique
Pena Nieto wa Mexico, sherehe zilizofanyika katika jiji la Mexico Jumamosi ya
Desemba Mosi 2012. Makamu wa Rais Dkt Bilal amekuwa miongoni mwa viongozi kadhaa
maarufu duniani walioshiriki sherehe hizo akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Joe
Biden.
Katika
sherehe hizo za kuapishwa zilizofanyika katika ukumbi wa Kongresi ya Mexico,
ukumbi ulio katikakati ya Jiji la Mexico, Rais Pena Nieto (46) aliapa na kisha
kuhutubia taifa huku akifafanua wazi kuwa, suala la kutunza amani na utulivu
katika Mexico ni agenda yake ya kwanza, huku suala la kukuza uchumi wa Mexico
likifuatia.
Rais
Nieto, katika hotuba yake hiyo alikuwa akizungumza kwa lugha ya ustahimilivu,
upole na uvumilivu, lugha inayotafsiliwa na wachambuzi wa masuala ya siasa wa
hapa kuwa, inalenga kuwatoa hofu wananchi wa Mexico kufuatia wengi hasa wakazi
wa mijini kuwa na hofu ya kurejea madarakani kwa chama kikongwe kabisa cha PRI,
kilichotawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 70 na kisha kudondoshwa mwaka 2000 na
Rais mstaafu Filipe Calderon.
Katika
hotuba hiyo pia Rais Nieto alizungumzia suala la kukabiliana na uhalifu, ambao
umekuwa ukiongezeka badala ya kupungua kadri siku zinavyoenda katika viunga
mbalimbali vya nchi ya Mexico. Katika miaka 6 iliyopita, watu wapatao 50,000
walipoteza maisha yao kutokana na matukio ya kihalifu na hasa ule unatokana na
makundi yanayojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Mexico ni moja ya
nchi duniani zinazokabiliwa na uhalifu wa hali ya juu hali ambayo Rais Nieto
anasema ameamua kukabiliana nayo, ili kila raia aweze kupita katika barabara za
nchi hiyo sambamba na miji ya Mexico akiwa na amani tofauti na ilivyo
sasa.
“Nitaheshimu
kila mwananchi, nitasikiliza kila hoja. Nitaendesha serikali kwa uwazi na
nitakuwa mkweli kwa wananchi wa Mexico. Nitatafuta maoni yenu na nitawasikiliza
wote bila kubagua. Nitakuwa Rais ambaye yuko karibu na wananchi,” alisema Rais
Nieto katika hotuba yake kwa Taifa.
Katika
sherehe hizi, Mheshimiwa Makamu wa Rais ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, sambamba na maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania
Washington. Wengine ni maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na mara baada ya shughuli hii, ujumbe wa Mheshimiwa Makamu wa Rais
unarejea nyumbani kukabiliana na majukumu mengine ya
kitaifa.
Tanzania
na Mexico zimekuwa na uhusiano wa siku nyingi uliohasisiwa na Hayati Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Uhusiano huu unachagizwa pia na hali ya
tamaduni na maisha ya wananchi wa nchi hizi mbili ambao wanafahamika pia kwa
ukarimu na tabia yao ya kupenda na kuthamini wageni.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment