Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa
waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa
Msaada wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja
wa Mataifa katika kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza
umaskini wakati wa Semina ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya
Haki za Binadamu tukielekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.
Mwezeshaji
wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa
changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha
jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa
nchini.
Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa
Mataifa kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za
mafunzo ambapo amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika juhudi
endelevu za kupunguza umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu
kulingana na visheni ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Mtalaam wa Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari
mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations
Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za
Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo
2015.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine
Mushi akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa
pamoja ‘Delivering As One’ na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi
hapa nchini.
Pichani Juu na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.
Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu
wa vyombo vya habari katika kutetea haki hizo na kufichua pale
zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.
Afisa Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony
Rutabanzibwa akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa
kuripoti masuala yanayohusu hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya
kazi zao.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti
wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa
semina hiyo akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya
habari inavyoweza kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki
za binadamu.
Afisa
habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama
akitoa changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na
mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za
kuelimishana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa
kufanya hivyo ndivyo watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa
Mataifa katika kupunguza umaskini na kutetea haki za binadamu.
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.
No comments:
Post a Comment