Tofauti na mastaa wengine ambao hupenda kujifichaficha kwa kutumia magari yenye vioo vyeusi ‘tinted’, mwigizaji ‘expensive’ wa filamu za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa laivu akikatiza kwa miguu, katikati ya Jiji la Dar, mitaa ya Posta.
Paparazi wetu alimfuatilia kwa muda mrefu, akampiga picha kadhaa (kama zinavyoonekana hapo chini).
Wakati zoezi la kumtandika picha likiendelea, kuna wakati mwigizaji huyo alionekana kama anataka kuomba lifti ya bodaboda lakini aliahirisha na kuanza kutimua mbio huku akiangua kicheko cha kiaina.
No comments:
Post a Comment