Monday, February 4, 2013

MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”

Meneja Mawasilianao wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (katikati) akiongae na waandishi wa habari hawapo pichani , wakati wa kuwakabidhi zawadi zao washindi zaidi ya thelathini  wa  Promosheni ya “MAHELA” inayoendeshwa na kampuni hiyo,zaidi ya shilingi milioni 400 zinaendelea kushindaniwa, kushoto ni Bw. Aghasese Mballa na kulia Bi.Ruth Mungure ambao wote ni wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja.
Mshindi wa Promosheni ya”MAHELA” Bi.Ruth Mungure,akikabidhiwa fedha zake  kiasi cha shilingi Milioni 1 na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa(kulia) wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zaidi ya 31 zawadi zao iliyofanyika jijini Dare Salaam, zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa, katikati ni Afisa bidhaa na huduma wa kampuni hiyo Bw.Athanasius Muhanuzi.
Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada na Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw. Charles Matondane pamoja na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw. Matina Nkurlu katikati wakimuangalia mshindi wa Milioni 1 Bw. Best Monuo wakati akihesabu fedha zake baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zaidi ya 31 zawadi zao iliyofanyika jijini Dare Salaam, zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
kutoka kushoto Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada na Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw.Charles Matondane,Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bi.Chiku Saleh pamoja na  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu wakifuatilia namba ya mshindi katika droo ya kumpata mshindi wa shilingi Milioni 5 katika promosheni ya ”MAHELA” inayoendeshwa na kampuni hiyo,zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”
Katika hali isiyo ya kawaida moja kati ya washindi wa promosheni ya” MAHELA” inayochezeshwa  na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania amebainisha kuwa utundu wa mtoto wake kuchezea simu umemuwezesha kushinda Shilingi milioni moja kutoka katika promosheni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa pesa hizo katika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo yaliyoko Mlimani City jijini Dar es Salaam,  Bi, Ruth John Mungule Mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amesema kuwa anaamini asinge kuwa mtoto wake kutumia ujanja kushiriki mchezo huo asinge weza kushinda pesa hiyo.
“Siku ya jumatatu asbui wiki iliyopita mtoto wangu aliniomba kutuma message ili kushiriki hii Vodacom MAHELA, nilimruhusu siku iliyofuata juma nne nilipigiwa simu kutoka Vodacom kuambiwa kuwa nimeshinda shilingi Milioni moja, haikuwa rahisi kuamini lakini hadi leo nimefika hapa na kukabidhiwa fedha zangu nimeamini ni kweli.
Mshindi mwingine alieshinda katika droo iliyo chezeshwa jana (jumatatu) ambaye ni askari polisi, Bi Liberata Karigita Mkazi wa Kilwa Road Balax, jijini Dar es Salaam, katika mahojiano yake kwa njia ya simu na Meneja wa mawasiliano wa Vodacom wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya pili alisema kuwa muda mwingi alipokuwa akiwasihi wenzake kushiriki walimcheka na kumbedha.
“Mala nyingi nilipokuwa nashiriki kwa kutuma message Askari wenzangu walinicheka na wengine kunibeza kuwa napoteza fedha zangu bure lakini leo Vodacom wamenitoa aibu na nimwshinda milioni tano nashukuru sana Vodacom, alibainisha Askari huyo.
“Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuitikia wito wetu na kushiriki vizuri katika promosheni yetu hii ya VODACOM MAHELA, Ninawasihi wateja wengine hata ambao hawajajiunga na Vodacomm kuhakikisha wanajiunga na kushiriki katika promosheni hii, MAHELA, ni kwa watanzania wote, alisema Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.
Hadi kufikia sasa tayari kampuni ya Vodacom kupitia promosheni yake ya Vodacom Mahela imepata jumla ya washindi 31 ambapo mshindi wa jumla atajishindia milioni 100 katika droo kubwa itakayo chezeshwa baada ya siku tisini za muda wa promosheni hiyo.

No comments: