Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo amepata mapokezi makumbwa mjini Kigoma mara baada ya kuwasili mkoani humo kwaajili ya kuhudhuria kilele cha Maadhimisho ya miaka 36 ya CCM yanayo fanyika kitaifa mkoani humo.
Rais Kikwete aliyeambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya pamoja na viopngozi wengine wa Chama hicho akiwepo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti bara, Komredi Philip Mangula, pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya chama hicho iliyokwisha kutangulia mkoani humo juma lililopita kwa njia ya reli ya kati.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na viongozi wa mbalimbali wa chama hicho waliofika kumpokea.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mwigulu Mchemba.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na viongozi wa chama tawala ambao ni marafiki kutoka Congo DRC
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na makada na Wanachama wa Chama hicho Mkoani Kigoma kutoka Familia ya Saratoga.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na Mzee Mwilima.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, na Rais Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akitazama
burudani ya ngoma kutoka kundi la Warumba Shauri la mkoani Kigoma. Anayepiga
Ngoma ni Mwajuma Hussein wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment