Tuesday, July 2, 2013

Azam yatua Bongo jana

azamtz 9ccc6
Azam (HM)
NYOTA watano wa kimataifa wanaokipiga katika timu ya Azam fc ya Dar es Salaam, maarufu kwa jina la wana lambalamba wanatarajiwa kuwasili nchini leo kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Azam na timu nyingine za Ligi Kuu, zimeanza kujiandaa na ligi hiyo itakayoanza Agosti 24.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Alhaji Idrisa Nasoro  amedokeza kuwa nyota hao wanaorejea leo wakitokea kwenye mapumziko ni Kipre Tchetche na Kipre Balou, raia wa Ivory Coast.
Aliwataja wengine ni Humprey Mieno, Joackim Atudo kutoka Kenya na Brian Umony wa Uganda, na kuongeza kuwa kuripoti kwa nyota hao ni faraja kubwa kwani mazoezi yataanza kunoga.
Mbali ya nyota wa kimataifa, pia wachezaji wengine wawili, David Mwantika na Omari Mtaki waliokuwa na udhuru, pia wanatarajiwa kuripoti leo.
Alisema mipango ya kwenda kujifua nchini Afrika Kusini kabla ya kuanza kwa ligi hiyo haijabadilika. Wataondoka mwishoni mwa wiki hii.
Alisema mipango ya safari hiyo inaendelea kupangwa na uongozi ikiwa ni pamoja na sehemu ya kufikia na mechi za kirafiki watakazocheza wakiwa huko.
Msimu uliopita Azam waliishia nafasi ya pili na hivyo kupata fursa ya kuliwakilsiha taifa katika michuano ya kombe la shirikisho. Chanzo: Baraka Mpenja

No comments: