Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es salaam
na baadaye akaongea na wanahabari
Obama akutana na rais Zuma
Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na
ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa
rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna
gani alivyo na utu wa kibinadamu.
Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha
ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao
uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Ziara hiyo ya bwana Obama ina lengo la kuongeza
mauhusiano ya kibiashara lakini imetekwa na hisia za ugonjwa wa bwana
Mandela ambaye amelazwa hospitalini kwa muda wiki tatu sasa kutokana na
maradhi ya mapafu yanayosumbua mfumo wake wa kupumulia.
Katika kikao hicho wawili hao walizungumza na
vyombo vya habari kuhusu ushirikiano wa mataifa yao kibiashara mbali na
kutafuta suluhu ya kudumu katika mataifa yaliokumbwa na ghasia mashariki
ya kati.
Ikulu ya White House imesema kuwa Obama pia atakutana na familia ya Mandela anayeugua maambukizi ya mapafu ili kuifariji.
Awali Rais Obama, aliye ziarani barani afrika alitoa shukran za dhati kwa uongozi ulioonyeshwa na Mandela.
Wakati wa ziara hiyo Obama pia atakutana na
wanafunzi huko Soweto kabla ya kuelekea katika jela la Robben Island
ambayo Mandela alihudumia kifungo chake cha miaka 27 wakati wa utawala
wa ubaguzi wa rangi.SOURCE: BBC SWAHILI
PICHA YA IKULU NA ISSA MICHUZI
No comments:
Post a Comment