Saturday, April 14, 2012

BABA MZAZI WA LULU AJITOKEZA NA KUSEMA YAFUATAYO

BABA MZAZI WA LULU AFUNGUKA

Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini  Lulu Michael a.k.a Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba,  ameibuka na kueleza kushtushwa  sana na  taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake. Baba Lulu,  ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo,  Mkoani Kilimanjaro, anasema kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini  masikio yake baada ya kupata  taarifa za kifo hicho,  huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.
Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya  Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe  April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba  alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya  Midway  mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17. Bw Kimemeta  alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao  kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama  baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu. “Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na  kusaidia katika kupatikana  kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu  Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake” alisema. Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni  ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa  wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji. “Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa  Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia  alikuwa ni mpenzi  - nilishtushwa” alisema Kimemeta. Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa  kushindwa kuhudhuria mazishi  marehemu  Steven Kanumba  kuhofia usalama wake, na kusema  mazingira  yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema  kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.

No comments: