Thursday, April 12, 2012

KATIBU TAWALA MKOA RUVUMA MPYA AONGEA NA WATUMISHI

Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko(aliyesimama) akiongea na watumishi wa ofisi yake hivi leo kufuatia kuteuliwa na Mh Rais Jakaya Kikwete kuongoza mkoa huo hivi karibuni.Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala Humphrey Paya.
 
Bi Sekawia Matimbwi akiongea kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma wakati wa kikao cha pamoja cha kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa (hayupo pichani).Tukio hili limefanyika leo katika ukumbi wa Maliasili,Songea
Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakisililiza maelekezo kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko(hayupo pichani).Kikao hiki kilikuwa cha kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa huyo kufuatia kuteuliwa na Mh Rais Kikwete kuongoza mkoa wa Ruvuma.
Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao ili kutoa mafanikio yanayotarajiwa na wananchi.
Rai hiyo imetolewa leo mjini Songea na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko wakati akiongea na watumishi katika kikao cha kufahamiana kufuatia uteuzi wake uliofanywa na Mh Rais Jakaya Kikwete mwezi uliopita.
 Bw Bendeyeko amewata watumishi hao kuhakikisha kazi znazofanyika zimekuwa na dhana ya Ushirikishwaji ili uamuzi wa pamoja katika ya Menejimenti na watumishi ndio iwe dira yao
“Chochote nitakachofanya nitapenda kufanya maamuzi katika vikao ili dhana shirikishi ifahamike vema kwa wote” alisema Katibu Tawala Mkoa na kuongeza kuwa maamuzi mengi nitakayopendelea ni kupitia makubaliano na maazimio ya Menejimenti tutakayotekeleza.
Aliongeza kusema ni vema watumishi wakawa na utamaduni wa kuheshimiana ,kuthaminiana na kushirikishwa katika mambo yanaendelea katika Ofisi.
Bw Bendeyeko aliwakumbusha wakuu wa sehemu na vitengo katika Ofisi yake kuwa na vikao na watumishi walio chini yao na kuwaeleza kwa uwazi juu ya hali inayoendelea katika Ofisi ikiwa ni pamoja na uwepo wa rasilimali fedha ili kila mmoja aelewa nakutekelza majukumu yake kupitia vipaumbele vilivyokubaliwa na wote.
Akiongea kwa niaba ya Wafanyakazi Bi Sekawia Mtimbwi ambaye ni Katibu Muhtasi alimpongeza RAS huyo kwa kuteuliwa kuongoza mkoa wa Ruvuma na kumhakikishia kuwa watumishi wapo tayari kumpa ushirikiano ili utekelezaji wa majukumu ya serikali uwe mzuri na wenye kuleta tija.
Bw.Bendeyeko ameteuliwa kuongoza Mkoa wa Ruvuma nafasi iliyokuwa wazi kufuatia aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa Bw.  Salehe Pamba kustaafu hapo mwaka 2010 .Hadi Mh.Rais Kikwete anamteua kushika wadhifa huo Bw Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments: