WANAUME WENGI HAWANA NGUVU ZA KIUME - MCHUNGAJI
Na Mwandishi Wetu
KIONGOZI mmoja wajuu wa dini amesema kwamba asilimia kubwa ya wanaume nchini hawana nguvu za kiume, hali iliyosababisha watoto wengi kuzaliwa nje ya ndoa.
Kauli iltolewa na Mchungaji wa Kanisa la Sauti ya Amani, John Kidoto wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kuwa wengi wa wanaume wenye tatizo hilo huanza kuona dalili mara baada ya kubalehe, au wakifikisha umri wa miaka 18 na kuendelea.
Kidoto alisema kuwa dalili za tatizo hilo huanza kujitokeza katika mfumo wa uzazi kwa kuanza kusinyaa wakati wa kujamiana,kuishiwa nguvu mara kwa mara,kuumwa mgongo, pamoja na kiuno.
Kidoto alibainisha kuwa kutokana na tatizo hilo limekuwa likisababisha ndoa nyingi kuingia katika migogoro ya mara kwa mara na hatimaye kuvunjika kwa sababu ya baadhi ya wanandoa kukosa uvumilivu huku wakishindwa kutambua kiini cha tatizo hilo.
“Nasikitika kwamba asilimia kubvwa ya wanaume nchini hawana uzazi kabisa na hili ni janga kwa sababu limesababisha familia nyingi kulea watoto wasio halali, na hali hii haiwezi kukubalika na kundi la wanaume hao”.
Mchungaji huyo alibainisha kwamba yawezekana tatizo hilo likachangiwa na nguvu za uchawi kwa kwa kile alichokiita kuwa ni nguvu za ‘majini’ kutawala mfumo wa uzazi wa mwanaume kwa kuhakikisha inaharibu au kuua uzazi wake mara baada ya kuingia katika ndoa.
“Kazi ya majini ni kuchochea uasherati ndani ya mwili wa mwanadamu kitu ambacho humfanya amsahau Mungu, na jamii imejenga imani kuwa majini huwalinda watu bila kufahamu madhara yake au nini maana ya ‘majini’.
Aidha, alisema ongezeko la tatizo hilo kwa kiasi kikubwa limechangia ndoa nyingi kujikuta katika misukosuko ambayo imekuwa moja ya sababu kuzitenganisha ndoa na kuwaacha watoto wakilelewa na mzazi mmoja kitendo ambacho si kizuri katika familia bora. hasa kwa kukosa uvumilivu ikiwa ni
No comments:
Post a Comment