Monday, April 30, 2012

Tundu Lissu Aanzisha Mashambulizi Mapya

Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi ya kesi
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
 Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akimtolea mfano muuza maji mjini Singida kwa kutumia toroli, maarufu kwa jina la 'Chai
Aprili 30,2012.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
Mnadhimu mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida, kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
Lissu ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri  wajiondoe mapema, badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza maisha yao.
Alisema kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa wanachama na viongozi wa chama hicho.
“Vita hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie sana,”alitahadharisha Lissu.
Kuhusu ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14 yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake utenguliwe.
Huo ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa, tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge, alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.

No comments: