Man City yarejea kileleni
Manchester City imechukua tena usukani wa ligi kuu ya England na kuongeza matumaini ya kunyakua ubingwa baada ya kuwachapa mahasimu wao Manchester United kwa 1-0.
Mpira wa kona katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza uliopigwa na David Silva uliunganishwa na nahodha Vincent Kompany na kumpita kipa David De Gea na kuandika ndio bao pekee lililodumu hadi mwisho.
Kipindi cha pili Manchester United walianza kwa kasi lakini Manchester City waligangamala na kuwadhibiti wageni.
Manchester City sasa wanaongoza ligi licha ya kuwa na pointi sawa na Man United, lakini wana idadi kubwa ya magoli.
Tofauti ya magoli kati ya timu hizo mbili ni 8.
Ushindi huu wa aina yake umekuja wakati ndoto za Manchester City za kuchukua ubingwa zikiwa zimekwisha fifia baada ya kufungwa na Arsenal mwanzo wa mwezi Aprili huku United wakiongoza kwa pointi nane.
Ligi hii huenda ikamalizika kwa chachu kubwa katika michezo miwili iliyosalia ambayo timu zote hazina budi kushinda iwapo zinataka kuweka matumaini ya kunyakua ubingwa.
Man City watakwenda kupambana na Newcastle kabla ya kuikaribisha QPR, huku United wakicheza na Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford kabla ya kusafiri kupambana na Sunderland katika mchezo wa mwisho wa
REFA: Andre Marinner
MAN UNITED LEO USIKU SAA 4:0 ZAIDI YA WATU MILIONI 650 KUANGALIA PAMBANO HILO. KILA TIMU YAJIGAMBO KIVYAKE ! YASEMWA NI DABI KUBWA
Sir Alex Ferguson na Wayne Rooney walipowasili kwenye mji husika
Ryan Giggs amecheza zaidi ya mechi 900 na huu mpambano anasema kazi ipo!!!
Hatima ya Ubingwa Ligi Kuu England Msimu huu inaweza kuamuliwa leo usiku wakati ile Dabi ya Timu za Jiji la Manchester itakapochezwa Uwanjani Etihad kwa Manchester City kukutana na Mabingwa watetezi Manchester United.
Tevez (kulia) ajiandaa kuanza badala ya Sergio Aguero(kushoto)
Vijana wa City: Joe Hart and Pablo Zabaleta wakikatiza kwenye mji City Centre jana jioni
Vijana wa Kazi Antonio Valencia, Javier Hernandez na Antonio Valenciana leo wanahitaji sare au ushindi ili kuusogelea Ubingwa wa kihistoria wa 20 huku Mechi zikiwa zimebaki 3 kabla ya Dabi hii.
Wakongwe wa Man U Ryan Giggs na Paul Scholes ni moja wachezaji wazoefu katika Tasnia hii ya mpira
Man City wao hawana ujanja na ni lazima waifunge Man United na hivyo kufungana kwa Pointi lakini wao watakuwa juu kwa ubora wa magoli.
Ryan Giggsni mmoja wa kiungo wa ukweli wa Man U japokuwa amekuwa achezi mara kwa mara
Mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana kwenye Uwanja wa Etihad Man United waliwafunga Man City bao 3-2 na kuwatupa nje ya Kombe la FA ambalo wao ndio walikuwa Mabingwa watetezi.
Kwenye Ligi Msimu huu, katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Old Trafford, Man United ilitandikwa bao 6-1 huku wakicheza Mtu 10 kwa muda mrefu wa pambano hilo.
Inasemekana kwa machungu ya Manchester City wachezaji walifanya mazoezi kwenye mvua
Kabla ya Mechi hiyo ya Ligi, Timu hizi zilicheza kwenye ile Mechi ya fungua pazia ya Msimu kugombea Ngao ya Hisani na Man United kushinda 3-2 baada ya kutanguliwa 2-0 hadi mapumziko.
Rooney na leo ataonyesha makeke yake tena au ...........
Katika Mechi 5 zilizochezwa mwisho Uwanja wa Etihad kati ya Timu hizi, Man United imepoteza Mechi moja tu.
[MECHI ZILIZOBAKI kwa Man United & Man City]
Man City | Man Utd |
Jumatatu Aprili 30 Man City v Man Utd Jumamosi Mei 5 Newcastle v Man City Jumapili Mei 13 Man City v QPR | Jumatatu Aprili 30 Man City v Man United Jumamosi Mei 5 Man United v Swansea Jumapili Mei 13 Sunderland v Man United |
Baada ya kumaliza kifungo chake cha Mechi 3, ‘Toto Tundu’ Mario Balotelli yupo huru kucheza Mechi hii lakini huenda Maneja wa Man City, Roberto Mancini, akaona ni bora awabakishe Mastraika wake toka Argentina, Sergio Aguero na Carlos Tevez, ambao wamekuwa wakicheza vizuri Mechi zao za hivi karibuni.
Nae Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, huenda akabadili Timu yake na mbinu ili kuhakikisha hawafungwi Mechi hii.
Wataalam wanahisi Fulbeki Rafael huenda asicheze na nafasi yake huenda ikakamatwa na Phil Jones au Chris Smalling.
Pia, kuna dhana kuwa Ferguson huenda akaamua kuweka Viungo watano kwa kuwajaza Ryan Giggs, Tom Cleverley au Park Ji-sung na hivyo kutomchezesha Danny Welbeck na badala yake wawe na Straika mmoja tu mbele-Wayne Rooney.
Pia, kuna dhana kuwa Ferguson huenda akaamua kuweka Viungo watano kwa kuwajaza Ryan Giggs, Tom Cleverley au Park Ji-sung na hivyo kutomchezesha Danny Welbeck na badala yake wawe na Straika mmoja tu mbele-Wayne Rooney.
VIKOSI VINATEGEMEWA KUWA NAMNA HII
Man City: Hart, Richards, Kompany, Lescott, Clichy, Milner, De Jong, Yaya Toure, Silva, Aguero, Tevez.
Man United: De Gea, Jones, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Scholes, Giggs, Park, Rooney.
REFA: Andre Marinner
No comments:
Post a Comment