Wednesday, April 18, 2012

VINGOZI WA CCM WAZUNGUMZIA KUHUSU JAMES OLE MILLYA

NA .ASHURA  MOHAMED -ARUSHA

Kufuatia Uamuzi aliyechukua hivi karibuni , aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha,Bw.James Ole Milya kutangaza kuhamia rasmi chama cha demokrasia na maendeleo Chadema akitokea CCM baadhi ya viongozi wa jumuiya hiyo pamoja na makada wa chama hicho mkoani hapa wamepokea kwa hisia tofauti uamuzi huo huku wengine wakidai wako njiani kuhamia Chadema.
Bw. Milya,alitangaza uamuzi wa kuachia nyadhifa zote ndani ya chama chake juzi huku akitumia nukuu za Rais wa awamu ya kwanza nchini hayati,Julius Nyerere kwamba CCM si mama wala baba yake.
Akizungumzia Uhamuzi huo wa Bw.Milya jana, Bi.Esther Maleko  ambaye ni Mwenyekiti wa Uvccm wilayani Arumeru mkoani Arusha alisema kuwa ameshtushwa na uamuzi wa Ole Millya kuhamia Chadema huku akidai kwamba tukio hilo limewachanganya vijana wengi ndani ya jumuiya yao.
Bi.Maleko alisema kuwa  uamuzi aliouchukuwa ulikuwa wakwake binafsi hivyo alikuwa na maslahi yake hivyo aliwaomba vijana mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi kutuliza akili zao kwa sasa wakati wakitafakari kitendo hicho.
“Mimi binafsi nimeshtushwa na uamuzi wake, vijana wengi kwenye kata wamenipigia simu wamechanganyikiwa hawajui la kufanya ila nawaomba kwa sasa watulie”alisema  Bi.Maleko
Kwa Upande wake  Mjumbe wa baraza la UVCCM mkoani Arusha,Bw.Kennedy Mpumilwa amemshangaa Bw.Millya kwa kusema kuwa hapandi gari lenye pancha kibao huku akidai kuwa badala ya kuziba pancha hizo yeye anakimbia gari lenye pancha na huko alikokwenda akikuta kunapancha atafanyaje

Alisema kuwa Millya  ametumia haki yake ya msingi  ya kikatiba kuhamia Chadema lakini kamwe kuondoka kwake hakutaathiri chama chao kwa kuwa ni chama kikubwa duniani na kina wasomi waliowengi
Alisema kwamba kiongozi huyo angeweza kubaki ndani ya CCM na kushirikiana na wao huku akisisitiza kwa kutumia msemo usemao kukimbia tatizo si kutatua tatizo.

 Katibu hamasa wa Uvccm wilayani Arumeru,Bw.John Nyiti alisema kwamba amesikitishwa na uamuzi wa kigogo huyo na  kudai  vijana wa CCM kutoka kanda ya kazkazini wametengwa na chama chao.
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa sana huyu alikuwa kiongozi mkubwa ndani ya chama lakini nikwambie vijana wa CCM kutoka kanda ya kazkazini tumetengwa na chama”alisema Nyiti

No comments: