Thursday, July 26, 2012

AZAM FC UBWINGWA NJE NJE 1 AU MBILI

AZAM FC YATINGA FAINALI YA KAGAME, INASUBIRI KATI YA YANGA AU APR JIONI HII

Mchezaji wa timu ya APR ya Rwanda Selemani Ndikumana akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Yanga Oscar Joshua katika mchezo wa nusu fainali unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, ambapo hakuna timu ambayo imefanikiwa kupata goli na tayari ni kipindi cha pili.
Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliokutanisha timu ya Azam FC ya Tanzania na Vita ya DRC Congo ni kwamba timu ya Azam FC imeifunga timu ya Vita magoli 2-1, hivyo kuifanya timu hiyo kusubiri mshindi kati ya Yanga na APR ili iungane naye katika mchezo wa fainali siku ya jumamosi Julai 28 kwenye uwanja wa Taifa.
 Wachezaji wa timu za Yanga na APR wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Kikosi cha Timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.

Mchezaji wa timu ya Vita ya DRC Congo akichuana na mchezaji wa timu ya Azam FC katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ambapo Azam FC imeshinda magoli 2-1 dhidi ya Vita ya DRC.

Mtangazaji maarufu wa mpira wa miguu katika kituo cha Televisheni cha Supersport Thomas Mulambo kutoka Afrika Kusini akiwapa maelezo kadhaa wataalam na wafanyakazi wenzake wa Supersport kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya APR ktoka Rwanda kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia baada ya mchezaji wao John Boko kuifungia timu yake goli la Kwanza.

No comments: