Tuesday, August 28, 2012

MGOMO WA MADREVA BUKOBA

 Ndani ya standi ya bukoba hamna gari dogo hata moja
 Makundi ya watu wanaosemekana ni madeleva wakiwa wanajadili juu ya mgomo huo,
 Baadhi ya watu wanaofanya biashara ndani ya standi wakiwa wamekaa bila kazi kwani hamna abiri wa kuwauzia bidhaa zao.
 Ni kundi kubwa la madreva lilijitokeza kufanya maojiano na mwandishi wetu
 Dreva akitoa kile alichonacho moyoni (Bora kufa njaa kuliko kuwafanyia kazi wazabuni wa standi hii)
 Dreva akiongea kwa uchungu mkubwa  mara baada ya kupewa majibu ya kuumizwa na mzabuni wa standi  ya kuwa wanajiangisha bure hamna kitakachofanyika juu ya hilo watarudi tu (aalisema dreva mmoja)
Madreva wakiongea kwa uzuni na hasira juu ya tukio hilo la kugoma kutoa huduma kwa wasafiri wamema :-
Wanashinikiza serikali kutimiza matakwa yao na kusema kuwa kiwango cha ela wanachotozwa kama ushuru wa standi ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha  standi haini vigezo maalum vya kuwa standi ya kulipia kiwango cha ushuru huo.
Inasemekana kuwa kwa siku gari moja aina ya haice,tax,pikipiki,mkokoteni  na hata gari binafsi linapoingia ndani ya stand  inaweza kulipa ushuru mpaka 4000/= kiasi ambacho ki kingi kwa maisha ya kaiwaida na ukilinganisha na athi ya standi yenyewe.

Wameendelea kusema kuwa wako tayari kufanya kazi na kukaa kwa mazungumzo na Mkrugenzi wa Manispaa ya bukoba kama alivyodai kuwa atakutana nao siku ya tarehe 01/08/2012.
Wameendelea kudai kuwa mpaka siku yenyewe ya tarehe 01/08 watakuwa tayari kuendelea kufanya kazi kama ungozi wa manispaa watatoa hamri kuwa kwa siku hizo tatu magari yote yasilipe ushuru ndani ya standi au yasingie ndani ya standi ila yaendelee kutoa huduma mtaani kwa kudaka abiria.

No comments: