Monday, August 27, 2012

VURUGU ZA FFU, CHADEMA MOROGORO, ZASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA

Mkurugenzi wa Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila akionyesha alama ya V wakati akiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU)
FFU wakiwa katika Doria.

Mwili wa aliyekuwa muuza magazeti katika eneo la Msamvu Morogoro, Ally Nzona ambaye alipigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia wakati wa vurugu za Polisi na Chadema Morogoro

Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro

Askari wa Kikosi cha kuzuia fujo FFU wakitoa onyo kwa waandamanaji kutawanyika

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege

Sehemu ya uamati wa watu Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege, Morogoro.
Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamani wa CHADEMA mjini Morogoro Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi.





Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya CHADEMA
Huyu ni mwananchi aliyeuawa na polisi kufuatia maandamano ya amani ya CHADEMA leo asubuhi... Alikuwa ni muuza magazeti ambaye hakujihusisha hata na maandamano. Wengine watatu wamejeruhiwa kwa risasi.

Makamanda wa chadema wakiwa kwenye dk 1 ya maombolezo kwa kumkumbuka kijana Alli aliyepigwa risasi na polisi leo Morogoro. (picha: Hosea D. Mtui's facebook wall)





Msimamo wa JOHN MNYIKA kuhusu vurugu, risasi, kujeruhi na “kuua” Morogoro!
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.
Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.
States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

No comments: