Monday, September 17, 2012

Mechi ya Prisons, Yanga yakosa mpira



Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza (katikati) akijaribu kuitoka ngome ya Prisons juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Na Khatimu Naheka, aliyekuwa Mbeya
KLABU ya Yanga imetoa msaada mkubwa kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutumia mipira yake kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons, juzi kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Wakati mchezo huo ulipotaka kuanza, mwamuzi aliwataka Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi waanzishe mpira lakini haukuwepo, hali iliyomfanya mwamuzi wa nne kwenda kuomba kwenye benchi la Yanga.
Mara baada ya ombi hilo, benchi hilo lilikubali kutoa mipira sita iliyotolewa na mtunza vifaa wa timu hiyo, Mahamoud Omari na kutumika mwanzo hadi mwisho wa mchezo huo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema hajajua tatizo lililosababisha uhaba huo wa mipira huku akiomba apewe muda amtafute Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba kwa ufafanuzi zaidi.
“Sina taarifa juu ya hilo lakini nipe muda nimtafute mkurugenzi wa mashindano ambaye anaweza kunipa majibu sahihi juu ya hilo,” alijibu Wambura.

No comments: