Msanii maarufu wa Rick Ross
kutoka nchini Marekani akishambulia jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 katika
viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo jijini Dar es
Salaam. Tamasha hilo kubwa la burudani nchini pia lilitumbuizwa na wasanii kibao
wa nyumbani.
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani
Rick Ross akiimba jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji
la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa
tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka
usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross imara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 201.
Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
Mwanamuziki kutoka nchini
Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa
wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku huu.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo
a.k.a Miduara,Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku
huu mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika
kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
No comments:
Post a Comment