Wednesday, October 3, 2012

WATU 3 WAFARIKI DUNIA, 24 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA RS WILAYANI KAHAMA



                                            Basi la RS katika muonekano wa ubavuni baada ya ajali.
 Muonekano wa lori ambalo limegongana uso kwa uso na basi la RS.…

                                            Basi la RS katika muonekano wa ubavuni baada ya ajali.
 Muonekano wa lori ambalo limegongana uso kwa uso na basi la RS.
 

Wananchi wakishudia ajali hiyo.
 Hii ndiyo hali halisi ya muonekano wa lori la kampuni ya Dhaudho baada ya ajali hiyo.
                                    Askari polisi akionyesha mguu uliokatika ukiwa ndani ya kiatu.
                     Miguu ya abilia iliyokatika  ikikusanywa na kuweka kwenye mfuko na askari polisi.
 Askari Polisi wakilinda amani na kuhakikisha vibaka hawaibi mizigo ya abiria, mkono wa kulia ni askari wa kike akiwa amebeba mfuko uliojaa miguu na viungo vingine vya abiria vilivyokatika.
                                 Baiskeli iliyosababisha ajali ikiwa imeachwa na mwenye nayo.
 Wauguzi wakiwa katika harakati ya kuokoa maisha ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
                                                  Majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu.
         Mmoja wa majeruhi ambaye amekatika mguu akipata huduma kabla ya kupelekwa hospitali ya Bugando.
Majeruhi aliyevunjika mguu akipata huduma ya kwanza.
 Kijana akimfariji jamaa yake ambaye amepata ajali.

 Wauguzi wa hospitali ya wilaya ya kahama wakiwa katika harakati ya kuokoa abiria ba kuwapa huduma ya kwanza.
WATU Watatu wamekufa papo hapo na wengine 24 wameruhiwa vibaya baada ya  Basi la Kampuni ya RS Bus Express linalofanya safari zake kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba  kugongana na Lori la Mizigo la Kampuni ya Dhaudho (Faw) katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama.
Ajali hiyo iliyotokea Katika eneo hilo ilihusisha Basi hilo lenye namba za usajili T 495 ATG pamoja na Lori lenye namba T 513 BNP ambalo likuwa likitokea Ushirombo Wilayani Bukombe mkoani Geita kwenda jijini Dar es Salaam majira ya saa 12.20 Asubuhi
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Emmanuel Endrew alisema kuwa mpaka kufikia majira ya saa nne za asubuhi tayari alikuwa amepokea jumla ya maiti tatu pamoja na majeruhi 24.
Alisema kuwa baadhi ya majeruhi wamevunjika miguu huku Wanne wakiwa mahututi na kulazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza kwa matibabu baada ya hali zao kuwa mbaya zaidi.
Kaimu Mganga Mkuu huyo aliwataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Edwin Stephano, Hamidu Yusuph ambaye alikuwa Dereva wa Lori la Mizigo pamoja na Zuraia Tuli (50) na kuongeza kuwa waliopelekwa katika Hospitali ya Bugando ni  Chabukana Raia wa Uganda, Makame Suleiman ambaye ni Mwanajeshi, Fred Peter na Shafii Abdalla.
Kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajali walisema kuwa kiini cha ajali hiyo kuwa, Dereva wa lori la mizigo alikuwa akimkwepa mwendesha Baiskeli hali ambayo ilisababisha lori hilo kwenda upande ambao basi ilikuwapo.
Hata hivyo mmoja wa Majeruhi wa Ajali hiyo Johanes Ndyamukamu alisema kuwa kabla ya ajali hiyo Basi hilo likuwa lifukuzana na jingine la Sumry ambapo baada ya kulipita walikutana na Lori jingine ambalo lilikuwa limemkwepa mwendesha Baiskeli huyo na kuingia katika upande wao.
Hata hivyo Kaimu Maganga huyo wa Haspitali ya Wilaya ya Kahama, Emamnuel Endrew alisema kuwa taarifa zingine atazitoa baadaye ili kujua kama kuna majeruhi wengine ambao watapatiwa ruhusa baada ya kupatiwa matibabu.

No comments: