Sharo Milionea enzi za uhai wake
Baadhi
ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za
usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki
Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam
kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo
Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule
Muheza Tanga.
Gari
aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa
akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo
Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga
Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na
mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Wakati
bado watanzania wakiwa katika majonzi na maombolezo ya kifo cha
msanii maarufu nchini Hussein Ramadhan a.k.a Sharo Milionea ,wadau wa
mtandao huu wa www.fourwaysbukobablogspot.com
wametoa tahadhari kwa wasanii maarufu hapa nchini na pamoja na watu
maarufu kuacha kutafuta kifo kama kilichomkuta Sharo Milionea.
Wadau
hao wamesema kuwa kifo cha Msanii huyo ni sawa na kifo cha
kukitafuta mwenyewe kutokana na kushindwa kutafuta dereva wa
kumwendesha na badala yake kuifanya kazi hiyo ya udereva huku
akitambua kuwa hana ujuzi wa kutosha wa kuifanya kazi hiyo.
Kwani
wamedai kuwa mbali ya kuwa bado hakuna anaeelezea chanzo cha kifo
cha Msanii Sharo Milionea ila uchunguzi wa awali unaonyesha taili
moja wapo la gari yake lilipasuka na kupelekea gari hilo kuhama njia
na kupinduka mazingira ambayo yanaonyesha wazi kuwa Sharo alikuwa
katika mwendo mkali na hakuweza kulimudu gari lake.
Hata
hivyo inasadikika kuwa katika fani hiyo ya udereva Msanii huyo kama
ameingia siku za hivi karibuni baada ya kuibuka na umaarufu na kuamua
kununua usafiri wake wa kutembelea.
Hivyo
wamedai kuwa iwapo angekuwa na dereva wa kumwendesha basi yawezekana
ajali isingemkuta ama hata kama ingemkuta basi yawezekana uhai wake
leo usingepotea.
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa wasanii wengi maarufu
hapa nchini hawajapitia kozi za udereva na pindi wanapopata fedha
wanakimbilia kununua
Wapo
wasanii wengi ambao siku za hivi karibuni wamepata kununua magari
yao na hivyo bila kuchukua tahadhali kwa kutafuta madereva upo
uwezekano wa ajali kama hizi kuendelea kutokea .
Hivyo
kuna haja ya askari wa usalama barabarani kunusuru maisha ya
wasanii wetu na watu maarufu hapa nchini ambao wanaendesha magari
yao kuwabana ili kuonyesha leseni zao na vyeti vya vyuo ambao wamesomea
udereva.
No comments:
Post a Comment