JK akiwaaga waombolezaji katika msiba wa Sajuki Tabata-Bima jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye msiba wa staa wa filamu Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo Rais Kikwete alifika…Stori: Imelda Mtema
MASTAA wa sinema Bongo wamejikuta katika hali ya kutoamini wanachokiona mbele yao kufuatia kukutana uso kwa uso na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwapa mkono wa salamu huku akiwachombezea kwa maneno mbalimbali, mengine ya utani, Amani linashuka nayo.
JK akiwaaga waombolezaji katika msiba wa Sajuki Tabata-Bima jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye msiba wa staa wa filamu Bongo,
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo Rais Kikwete alifika nyumbani kwa mjane wa
marehemu, Wastara ili kumpa pole.Nje ya nyumba ya Wastara iliyopo Tabata-Bima, Dar es Salaam, JK aliwakuta wasanii wamejipanga mstari kwa ajili ya kumpa mkono wa salamu lakini kila mmoja alishangaa namna rais alivyokuwa akiwafahamu mmoja mmoja walivyo au na kazi zake.
Msanii wa kwanza kukamata mkono wa JK alikuwa Yvonne-Cherly Ngatikwa ‘Monalisa’ ambapo rais alipomfikia alimwambia: “Noana sasa umekuwa mdada mkubwa.”
KWA DOKII
Alivyofika kwa msanii wa zamani wa Kundi la Nyota Ensemble, Ummy Wenslaus ‘Dokii’, Mheshimiwa Kikwete alimsamilia kwa zaidi ya dakika mbili huku akimuuliza ni kwa nini si mchangafu kama anavyomfahamu. Aidha, alimwambia anajua alikuwa anaumwa hivyo anahitaji muda mwingi wa kupumzika.
KWA DK. CHENI
Mcheza filamu huyu wa Bongo alishangaa sana aliposhikwa mkono na JK na kumtania:
“Unazidi kuiva tu, nimesikia mambo yako ni mazuri siku hizi ndiyo maana hunitafuti.”
AMFIKIA DUDE SASA
Alipofika kwa msanii aliyekuwa akiendesha Kundi la Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba ‘ Dude’, JK aliachia tabasamu pana na kumwambia amekuwa kimya na mambo yake hayaoni tena, hivyo akamtaka ajipange kurudi tena kwenye ‘gemu’.
KWA MIKE WA THEA
JK alimshika mkono Michael Sangu ‘Mike’ ambaye ni mume wa ndoa wa staa wa filamu Bongo, Misayo Ndumbangwe ‘Thea’ na kumsalimia kisha akamuuliza:
“Wewe vipi? Naona simu ya mkononi matukio yameisha au watu wameelimika nini?” (Simu ya Mkononi ni kipindi kilichokuwa kikirushwa hewani na Tv ya TBC1, Mike akiwa mshiriki).
SHUGHULI ILIKUWA KWA MZEE MAGALI
Katika mtiririko wa salamu hizo, rais alifika zamu ya msanii wa zamani wa Kundi la Sanaa la Kaole ambaye pia ni mcheza filamu mahiri kwa sasa Bongo, Charles Magali ‘Mzee Magali’.
Rais alimshika mkono na kumuuliza ni kwa nini amepotea, muda mrefu rais hajaona mambo yake. Japo lilikuwa ni swali, lakini Mzee Magali baada ya kuachana na mheshimiwa alirukaruka kwa furaha huku akisema alitamani mkono wa JK ubaki mikononi mwake.
Alisema haamini kama rais wa nchi anamfahamu yeye kama ndiye Magali anayeonekana kwenye filamu mbalimbali.
Hata hivyo, Rais Jakaya aliwasalimia wasanii wengine kwa tabasamu na kuonekana kuwa ni mmoja wa wadau wazuri wa filamu za Bongo kitendo kilichowapa farajav.
No comments:
Post a Comment