Sunday, January 20, 2013

SOKO LA BUKOBA KATIKA SIKU YA PILI BILA KUVUNJWA KAMA ILIVYOSEMWA AWALI


 Nilipozungumza na katibu mkuu wa wafanyabiashara hao Bwana DAVID DAMIAN, akasema kuwa wafanyabiashara wanasubiri kauli ya mahakama kwa kila jambo litakalojitokeza, kwani waliambiwa kuwa soko alipaswi kuvunjwa hadi kesi iliyopo mahakamani itakapomalizika.
Juzi tarehe 15 januari, Wafanyabiashara wa soko kuu la Bukoba waliazimia kukesha karibu na soko hilo, ili wahakikishe kama kutafanyika uvunjaji wa soko hilo, kama taarifa zilivyotolewa awali na baadhi ya viongozi wa manispaa.
Amesema kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tare 18 mwezi wa 3 mwaka huu.
 Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza nami, walionesha kuwa na wasi wasi  kuwa soko hilo lingevunjwa usiku wa kuamkia leo wakati  wa usiku, muda ambao hawatakuwapo sokoni hapo, hivyo inawezekana wakajikuta wakipoteza mali zao, lakini hatahivyo mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
Wamesema kuwa wanashindwa kuongeza bidhaa, kwasababu wanahofia kupata hasara ikitokea soko hilo likavunjwa.




Katika mikutano mbalimbali ya hadhara, wananchi walitangaziwa kuwa soko hilo litavunjwa tarehe ya leo 15 januari 2013, suala ambalo mbunge wa jimbo la Bukoba mjini na naibu waziri wa maliasili na utalii BALOZI HAMIS KAGASHEKI, aliwahakikishia wananchi hao kuwa ili soko hilo livunjwe lazima taratibu za kisheria zifuatwe.

No comments: