WANANCHI WA KITONGOJI CHA MKULILA WAUKATAA MRADI WA UMWAGILIAJI KISA HAWAKUSHIRIKISHWA HIVYO HAWAONI UMUHIMU WA MRADI HUO KIJIJINI HAPO
Moja ya wananchi wa ktongji cha mkulila akipiga mbiu ya mgambo wananchi wahudhurie kikao
Wananchi wakiwa tayari wamekusanyika kuwasikiliza viongozi wao
Mwenyekiti wa kijiji Tatizo John akifungua kikao
Diwani wa kata hiyo Noel Mwankwale akiwasihi wananchi hao kuwa wasikivu na kuukubali mradi huo lakini pia juhudi zake ziligonga ukuta baada ya wakazi hao kuendelea kusisitiza kuwa hawautaki kabisa.
Miongoni mwa watu waliozungumza katika mkutano huo na kuukataa mradi ni pamoja na chifu wa eneo hilo Michael Mwaifwani ambaye amesisitiza kuwa yeye kama chifu hajaona tatizo lolote katika mfereji huo.
WANANCHI wa kitongoji cha Mkulila kijiji cha Wambishe kata Ulenje wilaya ya Mbeya Mkoani hapa wamekataa mradi wa umwagiliaji uliopelekwa na serikali kwa madai kuwa hawakushirikishwa wakati wa uanzishwaji wa mradi huo ambapo pia wamesema hawaoni faida ya kuwa na mradi kama huo kijijini hapo.
Mradi ni kwa ajili ya umwagiliaji ulioletwa na serikali kwa gharama ya shilingi zaidi ya milion 40 ambapo wananchi hao wamedai kuwa mradi wa maji hautawasaidia chochote kutokana na kuwepo kwa mfereji unaotiririsha maji kwa kipindi chote cha mwaka.
Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ulioitishwa na Ofisi ya Wilaya kwa lengo la kuwaelimisha wananchi hao juu ya faida ya mradi huo jinsi utakavyowanufaisha kama kijiji na wananchi kwa ujumla.
Pamoja na Maofisa hao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mradi walipinga vikali huku wakidai fedha za meadi huo zipelekwe sehemu nyingine zakafanye kazi zingine.
Mkutano huo uliokuwa ukiongozwa na Maofisa Umwagiliaji kutoka Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ambao ni Malonga Msuya na John Kajange walijikuta katika wakati mgumu kutokana na mwitikio hafifu wa wakazi.
Hata hivyo Diwani wa kata hiyo Noel Mwankwale amewasihi wananchi hao kuwa wasikivu na kuukubali mradi huo lakini pia juhudi zake ziligonga ukuta baada ya wakazi hao kuendelea kusisitiza kuwa hawautaki kabisa.
Wamesema fedha hizo ni nyingi na kwamba haziwezi kutumika kujengea mfereji ambao hauna tatizo walamanufaa kwao kutokana na kutiririsha maji muda wote.
Miongoni mwa watu waliozungumza katika mkutano huo na kuukataa mradi ni pamoja na chifu wa eneo hilo Michael Mwaifwani ambaye amesisitiza kuwa yeye kama chifu hajaona tatizo lolote katika mfereji huo.
Mmoja wa wakazi hao Christian Matengere ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyeondolewa alisema ni vema wananchi wakasikilizwa na kutendewa vile wanavyotaka na siyo kuwalazimisha.
Amesema pia anasikitika kuona Serikali kutorudisha fedha zake alizokuwa ametoa kwa ajili ya kufungua akaunti ya benki kwa ajili ya mradi huo ambao alisema hauna maana yoyote.
Awali Maofisa hao wamesema lengo lao la kufika kijijini hapo ni kutoa elimu ambayo walikuwa wakiilalamikia kwamba hawakuipata kuhusu mradi na manufaa ya mfereji na kwamba hakuna shamba wala nyumba itakayoathirika wakati wa ujenzi wa mradi huo.
Aidha Mkutano huo ulifungwa pasipo kufikia muafaka wowote licha ya wananchi kuendelea kusisitiza kutouhitaji na kushauri kuwa mradi huo upelekwe kijiji cha jirani che uhitaji wa maji na sio wao.
No comments:
Post a Comment