KUSHOTO: Mandla Mandela. KULIA: Eneo la Qunu ambalo Mandela amesisitiza azikwe huko.
Mjukuu wa Nelson Mandela anatuhumiwa kwa kufukua makaburi kinyume cha
sheria na kuhamisha miili ya ndugu zake kutoka kwenye eneo la maziko la
familia hiyo.
Ndugu 16 wamemburuta mahakamani Mandla Mandela baada ya kuzika upya
mabaki ya miili ya watoto watatu wa baba huyo wa taifa mwenye miaka 94
mahali alikozaliwa huko Mvezo mwaka 2011.
Ugomvi mkubwa wa familia hiyo umeongezeka hivi karibuni na mashitaka
yalifunguliwa jana dhidi ya Mandla Mandela, huku babu yake akiendelea
kuwa katika hali mbaya hospitalini.
Ndugu wa Mandela wanadai Mandla Mandela hakuwa na ruhusa rasmi au hata kuwataarifu wanafamilia wakati akifanya maamuzi hayo.
Baba huyo wa taifa alishasema mapema kwamba anataka kuzikwa huko Qunu, ambako watoto wake walizikwa kwenye kiwanja cha familia.
Mandla Mandela alihamisha mabaki ya miili hiyo kwenda Mvezo, ambako anapanga kufungua hoteli.
Malumbano yalisikika Jumanne kuhusu amri ya mahamaka ikitaka miili hiyo kurejeshwa huko Qunu
Kesi hiyo inatarajiwa kumalizika leo.
Wakati huohuo, polisi walisema mashitaka ya 'kufukua kaburi'
yamefunguliwa dhidi ya Mandla Mandela kwa kuchimbua makaburi yenye miili
hiyo mitatu.
"Kesi imefunguliwa kwenye kituo cha polisi na sasa tutachunguza kesi
hiyo," alisema Luteni Kanali wa Polisi Mzukisi Fatyela, ambaye alikataa
kutaja nani aliyewasilisha mashitaka hayo.
No comments:
Post a Comment