Ngorongoro Heroes inaikabili Sudan kesho (Jumamosi) kwa staili ya kushambulia ili kuhakikisha inapata tiketi ya kusonga mbele katika michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 20. Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Uwanja wa Khartoum, jijini hapa kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo leo (Mei 4 mwaka huu), Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Kim Poulsen amesema kikosi chake ambacho jana usiku (Mei 3 mwaka huu) kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Omdurman kiko katika hali nzuri na kitatumia mfumo wa 4-4-2.
No comments:
Post a Comment