Saturday, July 7, 2012

KWA KUSEMA UKWELI MAISHA YETU YAMEBADILIKA SANA MARA BAADA YA KIFO CHA BABA WA TAIFA



 Ni wanaharakati niliobatika kukutana nao siku ya leo tarehe 07/07/2012 sabasaba day.
Nikiwa nasungumza nayo kwa njia tofautitofauti walinilazimisha kuwauliza hali ya maisha ya sasa.Sikuwa na budi ikabidi tuanze mjadara huo na kuacha malengo yangu pembeni.

Mdau:Kaka nakusitikia sana wewe mwenye umri mdogo kwani sisi walau tumekaribia kumaliza mkataba wa maisha yetu ila inaweza sababishwa na hali ngumu ya maisha iliyopo kwa sasa.

Mwandishi:KWani hii hali imeanza lini na kwanini unaona mabadiliko?

Mdau: Kwa kusema ukweli mimi maisha yangu yamebadilika tangu alipokufa baba wa taifa ndipo maisha yangu alipoanza kubadilika sio kuwa yeye ndo alikuwa ananitunza na familia yangu ila nasema kuwa kufa kwake walio wengi wamekutumia kama faida kwao kwani kwa sasa hawana wanayemuogopa.

Mwandishi:Ni akina nani hao ambao hawaogopi na wanatumia kifo cha baba wa taifa kuwa manufaa yao?

Mdau:Ni viongozi wa ngazi za juu wapo ambao hadi sasa  nikipewa nafasi ya kuwachapa naweza nikaua mtu  watu wanakula ela waziwazi na wala hata hawachukuliwi hatua yeyote hadi sasa inauma sana.

Mwandishi: Sa nini kifanyike?

Mdau:Ngoja tusubili 2015 kijana kila kitu nahisi kitakuwa sawa tu wala haina shida kwani kila chenye mwanzo si kina mwisho bwana.

Sawa bwana hamna shida mi naenda baba sawa.

No comments: