Monday, July 30, 2012

MGOMO WA WALIMU WASABABISHA WATOTO KUTAPAKAA NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA

 Wanafunzi wa shule ya msingi Makuburi manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,  wakiwa wameuchapa usingizi baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kufundisha bila mafanikio, wiki iliyopita Chama cha Walimu CWT kilitangaza kuwa leo jumatatu walimu wa shule za Sekondari na Msingi wangeanza mgomo nchi nzima kutokana na kutofikia muafaka kwa madai yao dhidi ya Serikali.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE) 
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabibo iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa wamelala baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kuwafundisha madarasani .

Ni katika manispaa ya mji wa Bukoba ambapo kila kona ya mji huu imetapakaa wanafunzi.
Hii ni kutokana na mgomo wa walimu kutokuwa kazini kwa siku ya leo jambo hili limepelekea wanafunzi kutumia nafasi hii kufanya wakitakacho kwani hawana uangalizi wa kutosha mara baada ya kuaga nyumbani kuwa wako shuleni.
Nikiongea na Mwalimu (jina limehifadhiwa) amedai kuwa yeye ni  mwalimu mkuu wa shule moja katika manispaa ya mji wa bukoba akiwa shule.
Amedai taarifa hizi za mgomo wa walimu amezipata mara baada ya mkuu wa chama cha walimu Tanzania kutangaza kuwa kutakuwa na mgomo wa walimu mapaka hapo itakapotangazwa tena kuacha mgomo huo .
Amesema kuwa mgomo huo ni wa kushinikiza serikali kutimiza madai yao mbali mbali yanayowahusu kama walimu.
Four ways bukoba itaendelea kuwalete habari kadri hali itakavyokuwa ................

No comments: