Monday, July 30, 2012

WALIMU MGOMONI LEO



Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl. Gratian Mukoba 
WALIMU nchini leo wanatarajia kuanza mgomo kuishinikiza serikali iwalipe madai yao mobilisable ikiwemo ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55 na asilimia 50 kwa walimu wa masomo ya sanaa.
Wakati walimu wakitarajia kuanza mgomo wa leo, serikali imetangaza kuwa mgomo huo ni batili kwa sababu shauri hilo liko katika Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi ya Rais (Ikulu), kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo, Julai 27 ilitoa taarifa kupinga mgomo huo kwa madai kuwa ni batili, kwa sababu kuna kesi mahakamani inayozihusu pande hizo mbili.
“Kwa sasa shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa Julai 27, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika mahakamani na mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne Julai 31, 2012 saa sita mchana ili kuiwezesha mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi. Kwa hiyo mgomo huo si halali kwa vile shauri hilo bado liko mahakamani,” ilisema.
Juzi Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alitangaza kuwa leo wangeanza mgomo nchini nzima huku akiwasisitiza walimu wasiogope kwa sababu taratibu zote za kisheria zimefuatwa.
Mukoba alisema Julai 28 (Ijumaa) mwaka huu, walimu walipiga kura ya kugoma au kutokugoma ambapo walimu 183,000 walipiga kura na 153,848 sawa na asilimia 95 waliunga mkono kufanyika kwa mgomo.
Alisema walifikia hatua hiyo baada ya serikali na CWT kushindwa kufikia makubaliano katika siku 30 walizoipa kuanzia Juni 25 mwaka huu.
Madai makubwa ya walimu katika mgomo huo, mbali na malimbikizo ya madeni yao ya huko nyuma, pia wanataka ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho za kufundishia kwa walimu wa sayansi asilimia 55 na walimu wa masomo ya sanaa asilimia 50 na posho za mazingira magumu asilimia 30.
Maandalizi yaendelea
Hadi jana jioni viongozi wa mikoa mbalimbali walitangaza kuunga mkono azimio la kugoma licha ya vitisho vilivyotolewa na sKatibu Mkuu wa CWT, mkoa wa Dar esSalaam, Abdallah Mkaula, aliwataka walimu wa mkoa huo kubaki majumbani kwao mpaka watakapotangaziwa vinginevyo na viongozi wao.
Mkaula alisema serikali imekuwa ikifanya jitihada za makusudi za kuwagawa walimu ili wasiwe na msimamo mmoja huku ikiendelea kukalia madai yao.
Mkoani Mara, Mwenyekiti wa CWT wa mkoa huo, Livingstone Gamba, aliwataka walimu wote kuanzia leo kutoenda kazini, ikiwa ni pamoja na kutokujaza fomu zitakazoletwa na mwajiri Gamba alisema kuwa matumizi ya nguvu yanayofanywa na serikali si jibu, bali utakomaza tatizo na walimu wasitishike na vitisho hivyo

No comments: