Friday, August 31, 2012

Mhe. Sitta katika ziara yake mpakani Mtukula- Kagera




GARI la afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Uganda aliyekuja kuungana na Mhe. Sitta katika ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki limepata ajali.

Gari la afisa huyo lilipata ajali lilipokuwa kwenye msafara wa waziri huyo uliokuwa ukitokea wilayani Karagwe ukelekea wilayani Kyelwa.

Ajali hiyo ilitokea muda wa saa 5:15 asubuhi katika eneo la Lukole katika Kata ya Ihanda baada ya gari la ofisa huyo wa ubalozi kuyumba na kuacha njia na kuangukia upande mmoja. Katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyeumia wote Ofisa wa Ubalozi na Dereva wake walitoka salama jambo ambalo halikuidhuru ziara ya Mhe. Sitta na kuendelea mpaka Wilayani Kyerwa Murongo.


Gari la Afisa wa ubalozi lililokuwa kwenye msafara wa Samwel Sitta lilivyopata ajali.




Wananchi wajaribu kulinyanyua gari la afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.



Samwel Sitta, akiangalia gari la ubalozi wa Tanzania nchini Uganda lililopata ajali kwenye msafara wake.



Maporomoko ya mto Kagera yaliyoko eneo la Kikakagati wilayani Kyelwa yatakayozalisha umeme utakaozinufaisha nchi za Uganda na Tanzania.


Samwel Sitta akiwa na ujumbe uliotembelea eneo la ujenzi wa mradi wa umeme utakaotokana na maporomoko ya mto Kagera.



Mhe. Sitta katika ziara yake mpakani Mtukula alitoa agizo kwa uongozi wa vijiji vya Mtukula pande zote Tanzania na Uganda kuweka utaratibu wa kutengeneza vibali ambavyo watendaji wa vijiji hivyo pande zote mbili watakuwa wanagonga mihuli na kumruhusu mwananchi kuvuka mpaka na kufanya shughuli zake na kurudi.


“Pamoja na kuongea na wananchi wa Mtukula Mhe. Sitta alitembelea na kukagua ujenzi wa jengo lmoja la kukusanyia ushuru ambalo llitakuwa na ofisi zote za ushuru na ukaguzi wa mpakani kwa pande zote mbili Tanzania na Uganda. Ujenzi wa jengo hilo unaendelea vizuri na linakaribia kumalizika ujenzi wake.

Mhe. Samweli Sitta pia aliwahakikishia wananchi wa mpaka wa Mtukula kuwa serikali imetenga shilingi bilioni kumi na mbili kwaajili kupeleka umeme katika mpaka huo wa Mtukula na vijiji vyote vinavyopatikana katika njia hiyo ya kuelekea Mtukula ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Aidha katika hatua nyingine Mhe. Sitta alisistiza wajasiliamali ambao wanaendesha biashara zao ndogondogo katika eneo la mpakani Mtukula kuwekewa mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao ili kujiinua katika hali zao za maisha.

No comments: