Thursday, October 4, 2012

Kampuni Ya China Yamshtaki Obama



Kampuni moja ya Marekani inayomilikiwa na Uchina imemshtaki Rais Barrack Obama kwa kuizuia kununua mashamba manne. 

 Mashamba hayo yaliyopo karibu na kambi ya Wanamaji katika eneo la Oregon, yalipangiwa kutumika kuzalisha kawi ya upepo .

 Kampuni hiyo, Ralls Corporation, inasema ni kinyume cha sheria na maonevu kwa Obama kutoa uamuzi wa kuizuia kununua mashamba hayo wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama. Kambi hiyo ya Wanamaji inatumika kufanyia majaribio ndege zisizo na marubani. 

Shirika la habari la Uchina limesema uamuzi huo wa Obama unahusiana zaidi na Uchaguzi wa Marekani kuliko masuala ya kiusalama. Hii ni mara ya kwanza kwa Mwekezaji wa kigeni kuekewa kikwazo nchini Marekani katika muda wa miaka 20.

                  Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

No comments: