JK Aongelea Vifo Vya Akina Mama UN
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waandishi wa habari hawapo
pichani, wakati wa uzinduzi wa mpango wa pili wa Ubunifu wa Uboreshaji
wa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto, katika maeneo ya vijijijni Nchini
Tanzania, mpango huo wa miaka mitatu unafadhiliwa na wafadhili
wawili, Meya ya Jiji la New York na philanthropies Michael Bloomberg na
Dr. Helle Agerup ambapo wamechangia dola za kimarekani milioni 15
kutoka kushoto ni Meya wa jiji la New York Michael Bloomberg, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na
Dr, Helle Agerup
Meya Michael Bloomberg, Ban Ki Moon, Rais
Jakaya Kikwete na Dr. Hellen wakiangalia video fupi iliyokuwa ikionyesha
kazi zilizofanywa za ukoaji wa akina mama wajawazito kwa kuwapatia
huduma ya upasuaji wa dharura, huduma ambayo imepatika kwa ufadhili wa
Meya na Philanthropies Michael Bloomberg ambapo kwa kupitia ufadhili
alioufanya kuanzia mwaka 2006 zaidi ya wataalam 106 wakiwamo wakunga na
manesi wamepatiwa mafunzo ya upasuaji wa dharura, pia huduma za afya
zimeboreshwa kwa kujenga au kuvifanyia ukarabati vituo vya afya na
zahanati katika ngazi za vijiji katika maeneo ya mikoa ya Pwani,
Morogoro na Kigoma. Ufadhili na kazi kubwa iliyofanywa na Bloomberg
pamoja na juhudi za Rais Jakaya Kikwete zimemvutia Dr. Hellen naye
kuwekeza nchini Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni anayetizama pembeni ni Katibu Mkuu Ban Ki Moon
Rais Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo
yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye naye
aliongoza ujumbe wake. Matukio hayo yote yamefanyika siku ya Jumanne
katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.
No comments:
Post a Comment